Watu Watatu Waliojifanya Wana Mafunzo ya Kijeshi Wasombwa na Mafuriko na Kufa

DODOMA: Watu watatu wakiwemo wawili ambao walijinadi kuwa wanamafunzo ya kijeshi, wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti ya kusombwa na mafuriko

Katika tukio la kwanza lililotokea kata ya Nzunguni, Diwani Aloyce Luhega, alisema kuwa katika eneo hilo watu wawili waliojinadi kuwa wanamafunzo ya jeshi walisombwa na mafuriko wakati wakitoka katika majukumu yao ya kazi majira ya jioni

Alisema watu hao walisomba na mafuriko walipojaribu kuvuka katika eneo lenye kivuko ambapo pamejengwa daraja la chini lililokuwa limejaa maji kutokana na mvua iliyokuwa inaendelea kunyesha juzi jioni.

Alisema miili ya marehemu imechukuliwa na Polisi kwa ajili ya hatua nyingine, ikiwamo walipotolewa na ndugu zao kuitambua. Pia aliwataka wananchi kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua

Alisema "Sasa hivi Polisi wanashughulikia suala hili, sisi kama Serikali ya Kata tumetoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuitafuta miili hiyo hadi kuipata"

Maoni