WAZIRI UMMY AIKABIDHI TIMU YA COASTAL UNION KIWANJA,AWAHIDI NEEMA

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameipongeza Kampuni ya City Plan kwa kuunga mkono juhudi zao za kutaka kuimarisha klabu ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya” kwa kuisaidia kupata kiwanja chao eneo la Maweni Jijini Tanga.

Hatua hiyo inatokana na viongozi kufanya kazi kubwa wakishirikiana na wadau kuhakikisha wanapambana ili kuiwezesha timu hiyo kurudi kucheza michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao baada ya kucheza madaraja ya chini kwa kipindi.

Kiwanja hicho ambacho kina ukubwa wa square mita 7632 kipo Mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambacho kina gharimu kiasi cha sh.milioni 38 kimepatikana baada ya kuwepo kwa juhudi kubwa za Waziri Ummy kuiomba kampuni hiyo kuisaidia timu hiyo eneo lake la kiwanja.

Kukabidhiwa kwa kiwanja hicho inafungua ukurasa mwengine wa mafanikio kwa timu hiyo kongwe hapa nchini.Akizungumza leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya kiwanja hicho, Waziri Ummy alisema kitendo cha kampuni hiyo kutoa eneo hilo kimesaidia mipango iliyokuwa nayo timu hiyo kuanza kwenda vema huku wakijipanga kwa hatua nyengine.

Alisema suala hilo linatokana na mshikamano uliopo baina ya viongozi waliopo wakiwemo wapenzi, mashabiki na wanachama huku wakiwataka kuuendeleza ili kuweza kupata mafanikio makubwa siku zijazo kwenye michuano ya ligi kuu.

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga katika akiwa na baadhi ya viongozi wa timu ya Coastal Union wakati akipokwenda kuwakabidhi kiwanja eneo la Maweni Jijini Tanga kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya City Plan Consultants (T) Limited Dkt Juma Mohamed

Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa ya makabidhiano hayo yaliyofanyika Mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni Jijini Tanga

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa timu ya Coastal Union akizungumza katika halfa hiyo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Tanga (TRFA) Saidi Soud kushoto akiteta jambo na Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga

Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji katika halfa hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa TRFA Saidi Soud na Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union Steven Mguto.

Maoni