WIZARA KUANGALIA NJIA SAHIHI YA UBORESHAJI UTOAJI HUDUMA ZA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJINI

Na John Nditi, Morogoro

WIZARA ya Maji na Umwagiliaji imesema ili kuleta  ufanisi mkubwa katika usimamizi  wa miradi ya maji safi na salama  vijijini, ipo haja ya kuwa na chombo cha kusimamia  huduma za maji vijijini utakaosimamiwa na wizara kwa lengo la kuleta uwajibikaji wa karibu kwa watumishi wanaosimamia sekta ya maji nchini.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Jumaa Aweso alisema hayo  kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali kikiwemo cha Dumila juu katika Kata ya Dumila, wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.

Kabla ya kuzungumza na wananchi  alipata fursa ya  kukagua ujenzi wa mradi wa maji Dumila  ambao ulianza kujengwa tangu Januari 24, 2014 na kukamilishwa Desemba 15, 2017 kwa gharama ya Sh milioni 800.5.

Naibu Waziri huyo alifanya ziara ya wiki moja  mkoani Morogoro  iliyomfikisha katika   halmashauri za wilaya sita  kati ya tisa ambazo ni  Malinyi, Ulanga, Kilombero, Mvomero, Manispaa ya Morogoro na Kilosa .

Alisema  kuwa,  miradi mingi ya maji safi na salama inayotekelezwa vijijini imekosa usimamizi wa karibu, ufanisi na mingi imejengwa chini ya viwango na baadhi katika maeneo ambayo vyanzo vyake vya maji si  vya kuaminika.

 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akisadia kuwapelekea mafundi wa ujenzi  kwa ajili ya  ukamilishaji  wa hatua za mwisho ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 150,000 katika mji wa Malinyi, ( kushoto) ni Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mkoani Morogoro, Dk Haji Mponda akichanganya saruji na mchanga kwa ajili ya ujenzi huo.

 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akisadia kuchanganya mchanga na saruji  kwa  ajili ya  ukamilishaji  wa hatua za mwisho ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 150,000 mjini Malinyi na ( kushoto kwake ) ni Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mkoani Morogoro, Dk Haji Mponda ,  na ( wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa wilaya hiyo Majura Kasika.

Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji , Jumaa Aweso,  akimsiliza Mzee Said Mazinge  wa  Kata ya Kibati, wilaya ya Mvomero , mkoa wa Morogoro  kuhusu changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama  alipofanya ziara  wilayani Mvomero. .

 Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaj, Jumaa Aweso akiwahutubia wakazi wa mji wa Mlimba , wilaya ya Kilombero  juu ya azma ya serikali ya awamu ya tano ya namna ya kutatua changamoto za ukosefu wa maji maeneo ya vijijini na mijini.

 Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaj, Jumaa Aweso  akipambu maji katika moja ya kisima kirefu  mara baada ya kukizundia katika kijiji cha Chikuti, wilaya ya Ulanga kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wa kijiji

Chanzo : MICHUZI.

Maoni