Yanga vs Kagera: Kamusoko kuanza, Cannavaro akiwa benchi


Kiungo Mzimbabwe Thabani Scara Kamusoko amechaguliwa kuanza katika kikosi cha kwanza cha Dar Young Africans kitakachocheza na Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu jioni hii.

Kamusoko anarejea kikosini baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha aliyokuwa akiuguza.

Katika kikosi hicho Nahodha Nadir Haroub Canavaro amepangwa kuanzia benchi sawa na Kipa Ramadhan Kabwili aliyeanza kwenye mchezo uliopita wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Township Rollers.

Kinachoanza: Youthe Rostand, Hassan Ramadhan Kessy, Haji Mwinyi, Said Juma Makapu, Kelvin Yondani, Patto Ngonyani, Emmanuel Martin, Thaban Kamusoko, Pius Buswita, Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib.

Akiba: Ramadhan Kabwili, Juma Abdul, Gadiel Michael Mbaga, Nadir Haroub, Makka Edward, Juma Mahadhi na Yusuf Mhilu.

Yanga watajitupa uwanjani kuwakaribisha Kagera Sugar katika mchezo wa raundi ya 21 utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Maoni