ZIARA YA MWENYEKITI UVCCM MKOA WA TANGA YAONDOKA NA UPINZANI.

Tarehe 12/03/2018 Mwenyekiti uvccm mkoa wa tanga ndugu Omari mwanga amefanya ziara wilaya ya handeni kata ya komkonga na kuongea na wanachama . 

Akihutubia mkutano huo, mwenyekiti wa vijana mkoa wa tanga amewataka viongozi waliochaguliwa na wananchi na watendaji wa serikali ngazi ya kata na vijiji kumuunga mkono mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa wao kuwa waaminifu, waadilifu na kutekeleza majukumu yao pasi na kumuonea mtu yoyote. 


Aliongeza kuwa viongozi wa chama cha mapinduzi ngazi ya mkoa hawatasita kuwachukulia hatua viongozi wa chama cha mapinduzi ngazi ya kata na vijiji itakapobainika wanakihujumu chama ama kufanya ubadhirifu wa mali za umma kwa namna yoyote ile. 

Nae, Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya handeni ndugu Athumani Marunda amewasisitiza wanachama kudumisha umoja, amani na ushirikiano katika kata hiyo ya komkonga. 


Katika mkutano huo aliyekuwa mwenyekiti wa chadema jimbo la handeni vijijini ndugu Omari Rashid Wazafa na viongozi wenzake wamejiunga na Chama cha mapinduzi. Akizungumza kwenye mkutano huo ndugu wazafa alisema uadilifu, uzalendo na utendaji kazi uliotukuka wa mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ndio kivutio pekee cha wao kujiunga na chama cha mapinduzi. 

Mwisho, mwenyekiti wa vijana mkoa wa  tanga ndugu Omari Mwanga alimpongeza mwenyekiti wa vijana taifa ndugu Kheri James  (MCC) kwa kazi anayofanya ya kujenga jumuiya ya vijana. 

Pia mwenyekiti wa vijana mkoa tanga amempongeza mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa uzalendo anaounyesha kwenye kuiongoza nchi yetu hakika vijana wanaimani kubwa na yeye.


Imetolewa na; 
Ofisi ya umoja wa vijana  (CCM)
Mkoa wa Tanga

Maoni