ZIARA YA MWENYEKITI WA UVCCM (W) KAHAMA

M/kiti wa UVCCM wilaya ya kahama Comrade SAMSON LUTONJA leo tarehe 07/03/2018 amefanya ziara ya kikazi katika kata ya Nyamilangano akiambatana na K/KATIBU UVCCM (W) comrade Raphael nyandi. 


Aidha M/kiti alimbata na M/kiti wa UVCCM wa wilaya ya shinyanga mjini comrade, DOTTO JOSHUA na M/kiti wa UVCCM wilaya ya Maswa comrade PAUL MASAGA kama wilaya rafiki.

M/kiti wa UVCCM aliweza kupanda miti katika shule ya msingi Nyamilangano na kukagua mradi wa ufugaji wa kuku katika shule hiyo uliofadhiliwa na shirika la EQUIP.


Sambamba na hivyo M/kiti aliweza kukutana na Baraza la Vijana la kata ya Nyamilangano ambapo aliweza kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili vijana zikiwemo ukosefu wa fursa za kiuchumi.

M/kiti aliwasii na kuwambia vijana kuchangamkia fursa za kiuchumi zitokanazo kwenye kata zikiwemo kilimo chenye tija na faida na kujiunga kwenye vikundi na kuazisha miradi ya maendeleo ili kuwaweza kujikwamua kiuchumi.

Pia aliwaasa vijana kuchangamkia na kuzitumia fedha zitolewazo na halmashauri ambapo ni 4% ya mapato ya ndani ya halmashauri ili kuwawezesha kukua kiuchumi na kuendana na ukuaji wa uchumi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais na M/kiti wa CCM Taifa Dr.JOHN POMBE MAGUFULI.


IMETOLEWA NA OFISI YA UVCCM (W) KAHAMA:
Raphael nyandi 
K/KATIBU UVCCM (W)
KAHAMA

Maoni