ZIARA YA MWENYEKITI WA UVCCM WILAYA YA BUNDA YAZIDI KUONESHA NURU

Ziara ya Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Bunda Ndg Gasper Charles akiambatana na Katiba wa UVCCM Wilaya Ndg Steven E. Shija wameendelea katika Kata Mbili ambazo ni Salama na Ketare ambazo zimekamilisha jumla ya Kata 16 kati ya Kata 33 za Wilaya ya Bunda

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ameendelea kugawa Vitendea Kazi kwa niaba ya Kamati ya Utekelezaji kwa Kata zote Mbili amewapa Muhuri, Kanuni na Daftari maalumu kwa ajili ya kuandikia Kumbukumbu za Jumuiya


Pamoja na kukutana na Baraza la UVCCM Kata, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya alikagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kata ya Salama, ambapo alitembelea kuona zoezi la kutoa Vyeti vya kuzaliwa kwa Watoto wa Chini ya Miaka Mitano, pamoja na Kukagua vilevile kushiriki Ujenzi wa Chumba kimoja cha Darasa katika Shule ya Msingi Kurusanga ambalo Darasa hilo linajengwa kwa ufadhiri wa Project Zawadi. 

"Tunawapongeza na kuwashukuru Project Zawadi kwa Ufadhiri huu, ni jambo jema mmefanya kusaidia Utekelezaji wa Ilani ya CCM Wito wetu Wadau wengine waige mfano huu" alisema Gasper. 

Vilevile Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya aliongozana na Viongozi wa Kata ya Ketare kwenda Kuhani nyumbani kwao na Marehemu Charles John ambaye alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Bigegu. 

Mwisho, Katibu wa UVCCM Wilaya aliwakumbusha Vijana kutumia Vikundi kuwa ndiyo Msingi wa mafanikio, Vikundi vyote vilivyopewa Mkopo na Halmashauri vilikumbushwa kurejesha Fedha hizo mapema. 

Imetolewa na :-
Ndg S.E.Shija
Katibu wa UVCCM Wilaya
Bunda, Mara

Maoni