CCM MAKETE WAUBOMOA UPINZANI,VIONGOZI CHADEMA NA CUF WAJIUNGA CCM.

Na Chriss Mbilinyi, Titho stambuli na Erasto kizumbe. 

Wilaya ya makete ccm (Half London)iliyobarikiwa kutuletea mwkt wa ccm mkoa wa Njombe mzee mwamwala  ,ikiongozwa na katibu wa ccm wilaya Langaely Akyoo na viongozi wa ccm wengine, utendaji wao wa kazi uliotukuka na uhodar wa watendaji na wakishirikiana na serikali, umeonesha kuwaridhisha wananchi wa makete kwa ujumla, kwani wameonekana kuwa watetezi na wasaidizi wa wananchi katika kushughulika na kero zao ,Hali iliyopelekea kuwavuruga wapinzani na kujitambua kwamba wao wanavuruga amani na mipango ya maendeleo ya wilaya ya makete na ccm ndio wanaoonekana kushika hatamu katika gurumu,.

Tafakari na shabaha yao imelenga mlango wa kulia na kusema kwamba mtoto kwa baba hakui, mchana kweupe walifunga kufuli milango yao ya ofisi ya chadema na CUF na kutimkia ccm huku wakilaani kupoteza muda wao, kwani wameishi huko muda mrefu bila mafanikio na kujikuta wakikosa amani.

Ambapo kiongozi wa chadema Agrey Mahenge akiwaongoza viongozi na wanachama wa chadema kutimkia ccm ,huku Mwkt wa CUF Dora Sanga akiwaongoza wanachama na viongozi wa CUF kutimkia ccm.

Hali imezidi kuwa mbaya makete kwani madiwani wanaotokana na upinzani wamezidi kubwaga manyanga na kuhamia ccm huku wakiwaomba samahani wananchi kwa kuwacheleweshea wananchi maendeleo, wasema sasa tupo tayari kuhakikisha makete inatulia na maendeleo yanapatikana kwa wakati. 

Wananchi wakiongea kwa nyakati tofauti na reporter wetu Chriss mbilinyi wameonekana kufurahishwa kwa namna ambavyo walikuwa wakikerwa na watu ambao walikuwa wakivuruga amani na maendeleo ya makete na kudai kama kuna watu wengine wamebaki mapema wajisalimishe la sivyo watakosa amani wenyewe kwani umoja na mshikamano uliopo ndani ya ccm unatosha kuleta maendeleo ndani ya makete.

Moto huo ambao umeendelea kuwakumba wapinzani kila kukicha, hatukuwa na budi kuuliza nini siri ya mafanikio kwa wanamakete hao, bila kumung'unya maneno wengi wao wakisema kazi kubwa ni kushughulika na kero za wananchi kwa ujumla, akionekana kuzidi kupanga mikakati zaidi katibu wa ccm wa wilaya hiyo langaely akyoo amewaomba wanaccm kuwa watulivu na kumpa ushirikiano wa kutosha kwani amejiandaa vyema huku akimfagilia mwkt wake wa ccm wilaya ya makete kwa ushirikiano ambao anampa huku akishukuru viongozi wenzake chama na serikali kwani siku hadi siku wameonekana kufanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na amani na maendeleo. 

ofisi ya siasa na uenezi mkoa wa Njombe, katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe unahabarika.

Maoni