DIWANI KATA YA MWAMKULU AOMBA TARURA KUNUSURU MIUNDOMBINU ILIYOZINGIRWA NA MAJI.

Diwani wa Kata ya Mwamkulu Kalipi  Katani amesema kata yake ipo katika hatari kubwa ya kimundombinu kutokana na barabara inayounganisha kata hiyo na maeneo mengine kuzongwa na mafuriko.

Akizungumza na Mpanda Radio Katani amesema adha hiyo imetokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kwamba sasa wananchi wanaendelea kuathirika na hali hiyo.

Katika hatua nyingine amesema baadhi ya makazi yameharibiwa na watu wawili wamepata majeraha baada ya kuangukiwa na nyumba.

Hata hivyo ameiomba mamlaka ya wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA Kuchukua Hatu za matengenezo ya barabara hiyo.

Kata Ya Mwamkulu ni miongoni mwa kata zinzoongoza kwa uzalishaji wa mpunga mkoani Katavi

Maoni