FURSA YA KUWAHOJI VIONGOZI KUMETUSAIDI KUPATA MAENDELEO -WANANCHI KATISUNGA

Wakazi  wa kijiji cha Katsunga Machimboni Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi wamesema wanapata fursa ya kuwahoji viongozi wao juu ya masuala mbalimbali ya maendeleo katika kijiji hicho.

Mpanda Redio imefika kijijini hapo ambapo wakazi hao wamebainisha kufika kwa viongozi wao mara kadhaa na kuwauliza kuhusu upatikanaji wa maji,zahanati  na umeme.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Lukas Kumpamba amesema wanapokea maoni ya wananchi kupitia sanduku la maoni na mikutano mbalimbali ya hadhara ambapo kwa sasa wako katika ufumbuzi wa changamoto ya zahanati.

Kijiji cha Katisunga Machimboni kina jumla ya wakazi 6000 kwa mujibu wa sensa iliyofanyika hivi karibuni kijijini hapo.

Chanzo:Ester Baraka.

Maoni