HUYU NDIO EDWARD MORINGE SOKOINE

Edward Moringe Sokoine alizaliwa tarehe 1 Agosti 1938 alikuwa Waziri 
Mkuu wa Tanzania tarehe 13 Februari 1977 hadi tarehe 7 Novemba
1980 tena akawa Waziri mkuu toka tarehe 24 February hadi tarehe 
12 Aprili 1984. 

Alikuwa ni mtu aliyependa usawa kwa kila mtu aliamini
kila mtu anaweza kuwa na maendeleo kama akijituma katika kilimo
na sehemu alipo pamoja na kujitegemea akiwa ni wakala wa 
mabadiliko katika nchi, mtu asielaumu na mwaminifu.

Alizaliwa Monduli Mkoani Arusha Tanzania, alipata elimu 
ya msingi na sekondari katika miji ya Monduli na Umbwe toka mwaka
1948 hadi 1958. 

Mwaka 1961 alijiunga na chama cha TANU 
baada ya kuchukua masomo katika Uongozi nchini Ujerumani 1962
hadi mwaka 1963. Aliporudi kutoka Ujerumani alikuwa Afisa Mtendaji 
wa Wilaya ya Masai, tena akachaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo 
la Masai. 

Mwaka 1967 alikuwa naibu waziri wa mawasiliano, usafiri
na kazi. Hatua nyingine katika maisha yake alijitangaza 
mpaka kuwa Waziri Mkuu 1970.

Mwaka 1972 alihamia kwenye Waziri wa usalama. Mwaka 1975 
alichaguliwa kwenye Bunge tena wakati huu kupitia Monduli.
Miaka miwili baadae akawa Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), 1977 alianza muhula wa kwanza ofisini akiwa 
Waziri Mkuu wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania. 

Muhula huu 
ulidumu hadi 1981, baada ya kutulia kwa kipindi cha mwaka alikuwa 
tena Waziri Mkuu tena mwaka 1983, alikaa mwaka mmoja ofisini
mpaka alipofariki Aprili 1984 kwa ajali ya gari. 

Kutokana na heshima na mchango wake kwa Taifa, kuna Chuo Morogoro 
Tanzania kilianzishwa kinaitwa jina lake (Sokoine University Of Agriculture (SUA)
kilianza mwaka 1984 kama chuo cha kilimo kinachotoa diploma
katika kilimo. Chuo hicho kikaongezwa hadi kutoa mchepuo wa
kilimo mwaka 1969 chini ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam. 
Tarehe kama ya Leo 12/04/1984 Taifa lilimpoteza kiongozi wake shupavu, aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine, kufuatia ajali ya gari eneo la WAMI-DAKAWA Kilomita 35 nje kidogo ya mji wa Morogoro. Waziri Mkuu huyu alikuwa akitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam baada ya kufunga Kikao cha Bunge mjini Dodoma.
Baada ya kuagwa kiserikali Jijini Dar, marehemu Sokoine alisafirishwa kwenda Monduli Juu Arusha kwa mazishi. 

Atakumbukwa kama kiongozi shupavu na ambaye alikuwa hacheleweshi utekelezaji wa jambo pale linapoonekana linatakiwa utekelezaji wa haraka na madhubuti.

Alipigana kupunguza rushwa na ufujaji wa mali, pia ulimimbikizaji wa mali mikononi mwa wachache (Ufisadi).
Sokoine alikuwa kiongozi wa mfano aliyekataa kujilimbikizia Mali bali alikubali kupunguza Mali zake ili aweze kuwatumikia vyema Watanzania.

Rapwi News Utataendelea kukumbuka daima na Watanzania kutokana na uzalendo, ushujaa na nia ya dhati ya ujenzi wa Taifa la Tanzania. Ni viongozi wachache sana nchini wenye roho na kariba kama yako.

Sokoine alikuwa kiongozi wa mfano ambaye daima alisimama upande wa umma.

Hakika, Edward Sokoine alikuwa kiongozi wa mfano wa kuigwa kwani aliishi kama ambavyo alikuwa akiyahubiri.

Maoni