JESHI LA POLISI GEITA LAMSHIKILIA MZEE WA MIAKA 69 KWA KOSO LA KUMUOA BINT WA MIAKA 13.

Jeshi la Polisi Mkoani Geita Linamshikilia Mzee wa miaka sitini na tisa (69) kwa kosa la kumuoa Binti wa Miaka kumi na tatu(13) ambaye anatokea kitongoji cha Rwenge Kijiji cha Bugalama. 

Mzee huyo ambaye anajulikana kwa jina la John Mkubila ambaye ni mkazi wa mtaa wa mwembeni kata ya Nyankumbu mjini Geita amekiri kumuoa binti huyo kwa makubaliano ya mzazi wa binti huyo kuwa awe anamsaidia kazi za nyumbani kutokana na mke wake kuwa na majukumu mengi ya kibiashara hali ambayo imepelekea kujikuta mzee akikosa huduma za msingi na kuamua kumuoa binti huyo. 

Aidha kwa upande wa Binti huyo amekiri kuolewa na mzee huyo kutokana na na Baba yake mzazi kumlazimisha.

Chanzo : Strom fm radio. 

Maoni