KAMATI YA RUFAA YA MAADILI YA TFF IMETUPILIA MBALI RUFAA YA WAMBURA

MASHTAKA YA WAMBURA

1. Kupokea fedha za TFF kinyume na taratibu  

2. Kulipwa malipo ya kampuni binafsi

3. Kushusha hadhi ya shirikisho.

UTETEZI WA WAMBURA

1. Kamati ya maadili ilikosea kisheria na kiuhalisia sababu haikuwa na mamlaka kusikiliza ushauri lake. 

2. Ilikuwa haiwezi kuthibitisha uamuzi wa kugushii.

3. Kamati haikuwa na baraka ya kamati tendaji.

4. Kamati ni batili maana makamu Mwenyekiti wake hakuna wakili.

5. Hapakuwa na ufuatiliaji wa kanuni za maadili za TFF hivyo kamati ya maadili haikuwa na mamlaka

6. Kamati kutoa uamuzi bila kumpatia nafasi ya kusikiliza yeye na muda wa kutosha kuleta utetezi wake.

7. Kamati ya maadili ilikosea kutoa hukumu wakati hapakuwa na ushaidi wowote uliupelekwa mbele yake.

8. TFF walishindwa kuthibitisha ushaidi kupitia kamati zake.

Hivyo uamuzi ule wote ulikuwa haram na batili katika shauri hili na anaomba kupitia wakili wake
Ndugu Lamwai kuwa

1. Itupilie mbali staka hilo

2. Aombwe radhi 

3. Alipwe gharama za kesho

4. Wapewe adhabu waliokiuka taratibu.

UTETEZI WA TFF

1. Mrufani alipewa muda na pia nakala za mashtaka yake na kufanya ndio maana alikuja mbele ya ndio

2. Mrufani alimtuma muwakilishi wake hivyo yote hayo ni haki ya kusikilizwa

3. Wakili mbele ya kamati walikubali kumuwakilisha mrufani hivyo hoja kuendelea.

4. Uchunguzi ulianzia ndani ya off na mrufani alijulishwa na akaenda kujijitea na akapeleka utetezi wake.

5. Kutokana na kosa lenyewe lipo wazi mno hakuna haja ya expert opion hivyo hapakuwa na lazima ya kutafuta nje ushauri ila kuna njia nyingine zinazosema kutumia katika kuthibitisha tuhuma. 

6. Ushaidi wa ripoti ya ukaguzi wa mahesabu inaonyesha wazi.

7. Wakati anapokaa fedha Wambura dola 30000 hakuwa na power of attorney ya kumpa uwezo wa kujua bali alikuwa na barua ya kawaida tu.

8. Kamati ilikuwa sahihi kwa kutumia kanuni zake

9. Wakili wa Wambura aliomba mteja wake afungwe angalau miaka 5 hivyo ni wazi kuwa ametenda kosa.

UPITIAJI WA KAMATI YA RUFAA

1. Wambura alipewa muda wa kutosha kusikilizwa.

2. Wambura alipewa haki ya zote na kamati ya maadili ilikuwa sahihi katika kuanza shauri hili.

3. Wambura alipewa taarifa za kutosha kuhusu shauri yake ikiwemo na ukaguzi wa mahesabu ya shirikisho.

4. Njia zilizotumika na kamati katika kujua kosa zinakubalika na zipo sawa ikiwemo na vielelezo viko sawa.

5. Hoja ya kuwa kamati haikuwa na mamlaka imeonekana kuwa kamati ina mamlaka kamili kuhusu mashtaka hayo yote.

6. Kamati ya maadili sio batili iko sawa

7. Kifungo cha maisha ya soka kwa Wambura iliyotolewa na kamati ya maadili iko sawa na iendeleee.

8. Kampuni iliyolipwa fedha ilikuwa mmiliki ni Wambura hivyo ni kosa kisheria mgongano wa maslahi ikiwa ni pamoja  kanuni za maadili za tff kupeleka mahakamani mambo ya mpira ikiwemo la club ya simba. Hivyo kamati hii imekubali tuhuma za kupokea fedha, kugushi barua za Wambura zako sahihi.

9. Kwa kuangalia mwenendo mzima toka 2002 hadi leo  Wambura katika kutumia  mbinu zote za ukwepaji wa umalizaji wa tukio hili ni kuwa Wambura hana mashiko kabisa 

10. Wambura alipewa haki zote za kusikilizwa na alipoona vitu vimezido akaanza kutuma muwakilishi hivyo kushiriki kila kitu mwanzo hadi mwisho.

MAAMUZI YA KAMATI YA MAADILI

1. Wambura atumikie adhabu zote alizopewa na kamati ya maadili

2. TFF wachukue hatua stahiki kisheria katika mashtaka haya kwa mujibu wa sheria.

Maoni