Kansela wa Ujerumani Angela Merkel aunga mkono mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa na Marekani,Ufaransa na Uingereza.


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema anaunga mkono mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa na Marekani, Ufaransa na Uingereza nchini Syria akiyataja muhimu na yanayostahili. 

Merkel amesema mashambulizi hayo ya angani yaliyofanywa leo asubuhi yanapaswa kuwa onyo kwa utawala wa Syria kutoendelea kutumia silaha za sumu. 

Rais wa Urusi Vladimir Putin amelaani vikali mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa na Marekani na washirika wake nchini Syria na kuitisha kikao cha dharura ckha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. 

Putin ameseam mashambulizi hayo ya angani yaliyofanywa mapema leo asubuhi na Marekani, Ufaransa na Uingerezan yanaufanya mzozo wa kibinadamu Syria kuwa hata mbaya zaidi na kuwasababishia raia dhiki na kuharibu mahusiano ya kimataifa. 

Rais wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk amesema Umoja wa Ulaya unaziunga mkono Marekani, Uingereza na Ufaransa kwa kuchukua hatua za kijeshi Syria dhidi ya utawala wa Syria unaodaiwa kutumia silaha za sumu dhidi ya raia wake.

Maoni