KATA YA KAKESE YAANZA UTEKELEZAJI WA ASILIMIA 10 KWA MAKUNDI MAALUM.

Kata ya Kakese iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imetekeleza mpango wa ugawaji wa asilimia kumi kwa vikundi vya wanawake na vijana.

Akizungumza na Mpanda Fm kwa njia ya simu afisa Mtendaji kata ya Kakese Lauben Kasomo amesema mapaka sasa shilingi milioni mbili zimetolewa kwa vikundi viwili vya wanawake .

Katika hatua nyingine amebainisha uwepo wa hamasa kubwa miongoni mwa wananchi katika kuunda vikundi kama inavyo takiwa na serikali kwamba ili kurahisisha utoaji huduma kwa jamii kwa njia ya vikundi.

Aidha ameongezea kuwa swala la ugawaji mikopo katika vikundi hivyo limekumbwa na changamoto nyingi ikiwemo bajeti kutokidhi mahitaji hasa kutokana na ongezeko la watu.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Mkaguzi mkuu wa wa hesabau za serikali Prof Juma Assad amezionya halmashauri kuacha kususua katika kutekeleza utoaji wa asilimia kumi kwa makundi ya vijana na wanawake.

Chanzo:Ezelina Yuda

Maoni