Katibu mwenezi ccm na katibu hamasa na chipukizi mkoa wa njombe waibeba njombe mji

Na Stambulititho, Njombe
Apr 02, 2018.

Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Ndg.Erasto Ngole pamoja na Katibu Hamasa na Chipukizi Ndg.Johnson Mgimba Mkoa Njombe wawataka wana Njombe kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao ya Njombe Mji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi hao wamewataka wananjombe kujitokeza kwa wingi uwanjani na  kuishangia timu yao ya Njombe Mji itakayo menyana na kalbu ya Simba ya jijini Dar es salaam hapo kesho Jumanne kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Njombe. 

"Ni vyema wananjombe tukaiunga mkono timu yetu  ya Njombe Mji na kuisapoti kwa nguvu moja ili kuhakikisha point tatu zinabaki nyumbani" - Katibu Mwenezi Ndg.Ngole alisema 

"Faida zinazoletwa na timu yetu ni kubwa sana asa ajira kwa vijana,biashara na kutangaza mkoa wetu wa Njombe kwa ujumla niwaase ndugu zangu wa mkoa huu wa Njombe kuisapoti na kuiunga mkono timu yetu " - Katibu Mwenezi Ndg.Ngole Alisema.
Na kwa upande wake Katibu Hamasa na Chipukizi Ndg.Mgimba amewataka wana Njombe kuwa wazalendo na kupenda vya nyumba na kuwataka pia wananjombe kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwatia moyo na morali wachezaji na timu kwa ujumla.

Maoni