KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE,APEWA BARAKA KIJIJINI KWAO,HUKU AKISEPA NA UPINZANI.

Na Titho stambuli Mtokoma na Erasto kizumbe.

Historia kubwa imeandikwa katika kijiji cha -Itulike, Kata ya Ramadhani, wilaya -Njombe ,Mkoa -Njombe.

Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Ndugu Erasto Ngole, Apr 08, 2018 ameweza kusimikwa na kupewa Baraka na wazazi, wanaccm, na Ndugu na jamaa kijijini hapo na Mkoa wa Njombe ukikusanyika kijiji cha itulike. 

Tukio hilo kubwa na la aina yake limesimamiwa na MNEC -Fidelis Lumato kuhakikisha katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe anasimikwa  kijijini hapo. 

Tukio hilo limeonekana kuvuta hisia za watu mkoani Njombe kutokana na sifa na umahiri wa kiongozi huyo ambapo watu mbalimbali wamesafiri kila pande ya mkoa wa njombe na nje ya mkoa wa njombe kuja kushuhudia tukio hilo, 

Mafuriko yalizidi kuwa makubwa pale msafara ulipowasiri kijijini hapo ambapo mapokezi makubwa yamefanyika kijijini hapo, Ngoma na kila aina ya burudani zilitawala kijijini hapo.

Viongozi mbalimbali wamehudhuria tukio hilo viongozi wa serikali wakiongozwa na Edwin Mwanzinga, Viongozi wa ccm wakiongozwa na MNEC -Fidelis Lumato na viongozi mbalimbali wa Dini wamehudhuliwa tukio la kusimikwa Ndugu Erasto Ngole. 

Ambapo Mh Edwin Mwanzinga amepata nafasi ya kutoa salamu kwa niaba ya madiwani amewaomba kumuunga mkono kiongozi huyo kwani ni mfano wa kuigwa kwa namna ambavyo anajituma katika shughuli za siasa na kilimo, aidha ameweza kulaani kitendo cha diwani wa kata hiyo anayetokea upinzani kushindwa kuiletea kata hiyo maendeleo, kwani ameshindwa kuwa mbunifu wa matumizi wa fedha anazo pewa na halmashauri ya mji kwa kuishia kununua bendera, photocopy machine na limu, huku shule  zikiwa na upungufu wa madarasa na hospitali,amewatahadharisha wananchi kutokuwaamin tena viongozi wanaotokana na upinzani na kutokuwachagua tena na kukiamn chama cha mapinduzi.Mgeni rasmi wa tukio hilo la kusimikwa kiongozi huyo Ndugu Fidelis Lumato amewaomba wananjombe hasa itulike alipo zaliwa kiongozi huyo kumpa nguvu na kuunga mkono jitihada za kiongozi huyo, pia amewashukuru wazazi, ndugu, na jamaa na marafiki kwa kuhakikisha wanakuwa na kijana mahiri Kama huyu ambaye ameibuka kuwa shujaa kwa mambo mbalimbali,amewaomba kuendelea kukiunga mkono chama cha mapinduzi kwani kimeonekana kuwatetea na kuwapigania wananchi wake hivyo hawanabudi kushikamana na kiongozi huyo kuhakikisha CCM inang'ara na kupata maendeleo .

Napia zoezi la kusimikwa likafuata na kufanyika kwa umahiri mkubwa sana chini ya MNEC -Fidelis Lumato, ambapo amekabidhiwa katiba ya ccm, ilani ya ccm, na kofia yenye nembo ya uanarakati.

Baada ya kusimikwa amewahutubia wananchi wa itulike na watu kutoka sehemu mbalimbali ,ambapo amewashukuru wanaccm kwa imani ambayo wamempa ya kuwa kiongozi wa ccm, pia amewashukuru wananchi na viongozi mbalimbali kwa kumpa ushirikiano wa kutosha na kuhakikisha kila jambo linafanyika kwa maslahi ya wananchi. 

Lakini pia amewaomba wananchi kutembea kifua mbele kwani yupo tayar kupigana nao kuhakikisha ccm inakuwa imara na inashughulika na kero za wananchi, wasijekutishwa na wapinzani Kwan kwasasa wamekosa mashiko na 2020 kata zote zitarud upinzan.

 

Lakini pia amewaahidi wananchi wa kijiji cha itulike atakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha umeme unawafikia kijijini hapo kwa kuwasiliana na idara husika. 

Amegusia pia swala la uchumi kuwahimiza wananchi kujihusisha na kilimo cha parachichi kwani kwa sasa ndio mkombozi wa uchumi kwa wananchi.

Baada ya hotuba hiyo viongoz na wanachama wa chadema walibwaga manyanga na kuhamia ccm kuunga juhudi za ccm na kuhakikisha wanaipoteza chadema

Kitengo cha habari tunakupongeza hakika Njombe imezizima kipande cha itulike. 

Imetolewa na ofisi ya siasa na uenezi mkoa wa Njombe.

Maoni