KATIBU WA UVCCM WILAYA YA LUDEWA ASHEREKEA PASAKA NA WATOTO WENYE MAHITAJI.

Katibu wa uvccm wilaya ya ludewa Ndg.Hassan kaporo, amesherekea sikuku vyema wilayan ludewa pamoja na watoto wenye mahitaji maalumu akishirikiana na watangazaji wa kituo cha Best FM, wameonyesha upendo wao kwa watoto hao kwa kusherekea pamoja nao na kutoa zawadi ya pasaka kwa watoto hao wanaolelewa katika Shule maalum ya Mundindi. 

Zawadi hizo ni Sabuni, Mafuta ya kupaka ,Dawa ya meno ,Daftari , na Nguo ,Licha ya kuwa ni siku ya kukaa pamoja na kusherekea na kuonyeshana upendo kwa kila mmoja, katibu wa uvccm alitumia fursa hiyo kuwapongeza na kuwashukuru wasimamizi na wanaotoa huduma katika kituo hicho kwani ni jambo la mhimu kuwasaidia watu wenye mahitaji hayo kwani wanahaki ya kupewa mahitaji kama watoto wengine. 


Pia ameweza kubaini changamoto zinazoikabili shule hiyo ni pamoja na Uhaba wa mabweni, kuna mabweni mawili tu na wanafuz wapo wengi ,Kwa ujumla changamoto ya miundombinu,kulingana na huduma muhimu itolewayo hapo shuleni, anawaomba wadau kuweza kujitokeza kuja kusaidia shule hiyo kutokana na umuhimu wa shule hiyo ili kuweza kuwasaidia watoto hao wanaohitaji kupatiwa elimu kama watoto wengine.

Ndg.Hassan kaporo amewaomba vijana na jamii nzima katika kuadhimisha sikukuu za kidini ni vyema wakawa wanakumbuka kufanya matendo ya huruma hasa kuwasaidia wasio jiweza na wanaohitaji mahitaji maalumu,Badala ya kufanya sherehe kubwa huku wapo watu wasioweza hata kula chakula kwa siku milo mitatu, akisisitiza kufanya  ibada na matendo ya huruma.

Aidha ameahidi kuendelea kuwapa ushirikiano yeye pamoja na ofisi yake katika makundi hayo kwani yanahitaji msaada wa karibu sana kulingana na hali yao ili kuweza kuwafanya waonekane Kama hawajatengwa,huku akiamini binadamu yeyote Mwenye imani yake ya kweli hili jambo ambalo hata dini zetu zinasisitiza ni moja ya sadaka kubwa na matendo ya huruma. 
  

Imetolewa na Titho stambuli Mtokoma na Erasto kizumbe, kutoka ofisi ya siasa na uenezi Mkoa wa Njombe. 

Maoni