KATIBU WA WAZAZI WILAYA YA WANGING'OMBE  AWAKUMBUKA WATOTO YATIMA WENYE MAISHA MAGUMU SIKU YA MAADHIMISHO YA WAZAZI CCM .

Na Titho stambuli Mtokoma na Erasto kizumbe. 

Uwezo, umahiri na uhodari wa Katibu wa wazazi wilaya ya wanging'ombe Ndugu Juma nambaila ameongoza Jumuiya ya wazazi wilaya ya wanging'ombe katika kuadhimisha siku ya wazazi ccm kiwilaya yaliyofanyika Tar 04/04/2018 Katika Kata ya uhenga ,kama ilivyokawaida yake ya kutambua yeye ni mzazi amejikita zaidi katika kuhakikisha swala la malezi ya watoto yanakuwa salama na kuhakikisha watoto ambao wapo katika mazingira magumu wanasaidiwa ili kuweza kutimiza ndoto zao.

Katibu huyo umejidhihirisha pale alipomudu kuhakikisha maadhimisho hayo yanaenda sambamba na ajenda kubwa ya malezi ndani ya jumuiya hiyo. Malengo ya Katibu huyo ndugu juma nambaila ni kuhakikisha umoja wa wazazi unakuwa na nafasi kubwa ya kurejesha tumaini la watoto ndani ya jamii. 

Katika siku hiyo ameweza kuongozana na wajumbe wake kutembelea Shule ya msingi uhenga na ikulimambo zote za kata ya uhenga  wilaya ya wanging'ombe,na kuwapa vifaa vya shule watoto yatima na kuwasisitiza kukazana kusoma ilikuweza kujinasua katika hali ya maisha inayowazunguka watoto hao, huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali kuweza kujitokeza na kusaidia kundi la watoto Hao kwani wanategemea zaidi furaha kutoka kwa walezi wao, licha ya kufurahi kuwafikia watoto huzuni inatokea ambapo unawaacha peke yao na kubaki wakiwa peke yao bila kujua hatima yao huko waendako majumbani.

Ubunifu na mipango ya katibu huyo haikuishia hapo Licha ya kufanya zoezi hilo wazazi waliamua kujihakikishia usalama wa afya zao katika kituo cha afya kata ya uhenga, kwani wao Kama wazazi wanawajibu wa kuhakikisha swala la afya katika jamii linasimamiwa vyema ,kwani wanaamin katika jamii afya ndio mtaji wa kwanza ,ili kujihakikishia nguvu kazi katika jamii ni lazima taifa lijihakikishie wananchi wanakuwa na afya kwa kuwapa elimu ya afya wananchi na wajikite katika kupambana na magonjwa mfano malaria ,HIV na magonjwa ya kuambukiza, amewaomba wataalamu wa afya kuhakikisha wanatimiza vyema wajibu wao.

Ndugu juma nambaila licha ya majukumu hayo amekumbuka kuwa yeye ni mawanasiasa na anawajibu wa kuhakikisha kipande cha wanging'ombe ccm inakuwa imara kwa kuhakikisha wanapambana na kero za wananchi, ametoa wito kwa wanaccm na wananchi kwa ujumla wanashirikiana vyema kutatua kero zinazoikumba jamii, Pia amewaomba wananchi kuunga mkono juhudi za awamu ya tano kwani raisi amedhihirisha kuwa anania ya kweli katika kuhakikisha taifa linasonga mbele, amewaomba wananchi kuwa karibu na viongozi na kuwapa ushirikiano ili kuweza kubaini changamoto na kuzitatua kuliko kupiga kerere bila sababu kwani wanauwezo wakueleza nini kinawasibu na wakasikilizwa kwani awamu ya tano imeonekana ni ya mipango zaidi na kuhakikisha inatimiza ndoto ya kuhakikisha kila mmoja ananufaika na rasilimali za nchi hii.

Ametoa wito yeye na ofisi yake watazd kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wananchi ili kuweza kuhakikisha ccm inakuwa imara na kuendelea kushinda kila chaguzi na kujikita kuhakikisha uongoz bora na uliotukuka. 

Akiongea na mtandao wa habari ameweza kutoa shukrani za dhati kwa mwkt wake kwani amekuwa akimpa ushirikiano wa kutosha katika utendaji wake,pia amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao kwani amekuwa akishirikiana na makundi mbalimbali bila kujali itikadi za kisiasa amewaomba waendelee hivyo kwani imani kwa ccm inazidi kuongezeka kila siku. 



Habari hii imepewa nguvu na ofisi ya siasa na uenezi mkoa wa Njombe  ......shikamoo parachichi anahakikisha unahabarika tunakufikia popote ulipo.

Maoni