KILAKALA ATOA SALAMU ZA PONGEZI KWA VIONGOZI WA UVCCM WILAYA.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa DAR ES SALAAM Ndg. MUSSA KILAKALA kwa niaba ya Ofisi ya Jumuiya ya Vijana Mkoa anatoa salamu za Pongezi wa Viongozi wote wakuu wa Jumuiya ya Vijana katika  Wilaya zote za Mkoa huu,  Wilaya hizo ni KINONDONI, UBUNGO, ILALA, TEMEKE na KIGAMBONI.

Mwenyekiti amepongeza Viongozi hao wa Jumuiya kutokana na kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka kuhakikisha Jumuiya inazidi kuimarika katika nyanja zote Mkoa wa Dsm.

Mwenyekiti aliwapongeza kipekee  viongozi wa Wilaya kama wafuatao:-

1. Ndg. Ahmadi Pazi na Irene Mollel na Muhasishaji wao Mtumwa Ligele Fadiga kwa kazi nzuri Wilaya ya Ilala.

2. Lilian Mkotani, Rashid  Semindu na Muhamasishaji Salum Viduka kwa Wilaya ya Kinondoni.

3. Fadhil Famonga, Jamal Khimji na Muhamasishaji Ngajua kwa Wilaya ya Temeke.

4. Edwin Mrema, Leah Mbeke na Muhamasishaji Tausi Hassan kwa Wilaya Ubungo.

5. Mathei Mponela, Twalib Belege na Muhamasishaji A. Mbunga.

Kwa hakika viongozi mnafanya kazi nzuri mnastahiki pongezi kwa kufanya Ziara katika Matawi na Kata zenu lakini pia kuwavutia wapinzani na vijana ambao hawana vyama kujiunga na Jumuiya yetu pamoja na CCM kwa ujumla.

"Aidha niwapongeze Vijana wa Kinondoni kwa kupambana usiku na mchana kuhakikisha chama kinashinda chaguzi ndogo za Mitaa zilizofanyika jana"

"Hakika sasa Dsm ni ya CCM hongereni sana kwa ushindi"... alisema Mwenyekiti Kilakala

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

Imetolewa na Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Mkoa wa DAR ES SALAAM.

Maoni