MANISPAA YA UBUNGO KUWANEEMESHA WAFUGAJI, KUTENGEWA  ENEO RASMI KWA AJILI YA KITUO CHA UKUSANYAJI MAZIWA.

Hayo yamezungumzwa leo kwenye uzinduzi wa jukwaa la wafugaji kwa manispaa ya Ubungo uliofanyika katika Ukumbi wa Manispaa Kibamba ambapo mgeni rasmi alikuwa Kaimu DAS bi Diana Kalumuna ambae amemuwakilisha Mkuu wa Wilaya Mh.Kisare Makori.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mgeni Rasmi ndg.Diana Kalumuna amewahakikishia wafugaji hao kwamba yuko pamoja nao katika kuhakikisha wanafikia malengo yao.Aidha aliwataka kuzingatia sheria zinazohusu sekta hii ya mifugo ambazo ni sheria ya magonjwa ya wanyama Na.17ya mwaka 2003,sheria ya nyama Na.10 ya mwaka 2006,sheria ya biashara ya ngozi na mazao yake Na.18 ya 2008 na sheria zingine.

Nae Mwenyekiti wa UJUWA akisoma risala mbele ya mgeni rasmi wameomba kusaidiwa kuanzishwa kwa duka la madawa la serikali ili kuepuka na gharama kubwa katika maduka binafsi pamoja na kituo cha kuuzia maziwa ombi ambalo tayari limeshafanyiwa kazi ambapo ameeleza kaimu Mkurugenzi Ally J.Ally kwamba Manispaa ipo kwenye mchakato wa kutenga  eneo maalum kwa ajili ya wafugaji litakalotumika kwa ajili hiyo kama kituo cha ukusanyaji maziwa. 
Katika hatua nyingine Mkuu wa kitengo cha mifugo ndg.Mgonja amewataka wanachama wa UJUWA kuwatumia wataalam wa manispaa bila kusita katika matatizo wanayokutana nayo na kwamba wako sambamba nao kuhakikisha wanafikia malengo yao.
Jukwaa hili la wafugaji linajumuisha  wafugaji waliopo katika kata zote 14 za wilaya ya Ubungo.

Hongera wafugaji kwa kuanzisha UJUWA.(Ubungo Jukwaa la Wafugaji) kwa kuzindua rasmi jukwaa lenu.

Sekta ya Ufugaji huliingizia Taifa Pato kwa asilimia 4.4.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO MANISPAA YA UBUNGO.

Maoni