MBUNGE VITI MAALUMU KUTOKA MKOA WA NJOMBE ATEGUA MTEGO NA KUBEBA NJOMBE BUNGENI. 

Titho stambuli Mtokoma na Erasto kizumbe 


Malkia wa Nguvu sio lazima atengeneze kitu, uwezo wake wa kufikiri , uhodari, na kusimamia jambo inatosha kuwa Malkia wa Nguvu. 

Mheshimiwa Neema Mgaya ni Malkia wetu wa Nguvu, Licha ya kusifu juhudi za Mheshimiwa raisi Bungeni na kumpongeza kwa kazi nzuri anayofanya ameonekana kusimama kidete wakati akichangia hoja bungeni kwa kuikumbusha serikali kuwajibika katika kutatua changamoto zilizopo ndani ya mkoa wa Njombe.

Mtu kwao ni msemo lakini leo mheshimiwa Neema Mgaya pale alipo wasilisha hoja zenye mashiko kwa maslahi ya maendeleo Njombe na Kwa ustawi wa jamii ya wananjombe ameikumbusha serikali juu ya hali ya afya, uchumi na Elimu. 

Ambapo ameweza kuipongeza serikali kwa kuweza kuleta dawa kwa 90% ,lakini kunachangamoto kwa kutokutosheleza kwa kuwa hospital kama makambako inachukuliwa Kama kituo cha wakati mwaka 2013 ilipandishwa hadhi kuwa hospital hivyo ameikumbusha serikali kuweza kuangalia upya juu ya budget ya hospital hiyo, lakini pia ameikumbusha serikali kujenga hospital ya wilaya wanging'ombe, Njombe DC na pia kukarabati hospital ya wilaya kwani kwa sasa inategemewa Sana hivyo inahitajika ukarabati,mheshimiwiwa Neema Mgaya ameiomba serikali kutupia macho swala la Afya kwani ni muhimu sana katika jamii yetu kwa kuwa mtaji wa kwanza katika jamii ni Afya hivyo ameiomba serikali kushughulikia hilo. 

Pia hakuishia hapo bado akapambana kuikumbusha serikali changamoto zinazoikabili Elimu mkoani Njombe ambapo ameikumbusha serikali kuwa Njombe inakabiliwa na upungufu wa Madarasa, upungufu wa walimu wa sayansi huku akiibeba zaidi ludewa kwa kuweka wazi uhaba wa walimu 521,ameitahadharisha serikali kuwa mfumo wa elimu ili uwe bora ni lazima miundo mbinu na walimu ili kuweza kuboresha kiwango cha elimu mkoa wa Njombe.

Pia ameweza kuikumbusha serikali juu ya malipo ya mawakala wa mbolea ambao hawajalipwa na serikali tangu 2015-2016 ,amewapigia magoti kuomba walipwe ili waweze kuendelea na shughuli zao. 

Hakuishia hapo mbunge huyo machachari kwa kutambua uchumi wa Njombe asilimia kubwa wanategemea kilimo ,ameiomba serikali kuhakikisha wanamaliza tatizo la changamoto za pembejeo za kilimo kwa wakulima kwani kilimo ni uti wa mgongo katika mkoa wetu Wa Njombe, Ili kuweza kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo ni lazima pembejeo ziwe karibu na wakulima na kuwa na bei nafuu ilikuweza kumudu gharama na kuzalisha chakula cha kutosha Kwa kuweza kusaidia na mikoa mingine kwani endapo pembejeo zinapatikana kwa urahisi na uzalishaji utakuwa juu.

Kilio kingine kwake bungeni ilikuwa ni changamoto ya maji katika mkoa wa Njombe ambapo ametaja maeneo kama lupembe, Njombe, makete na makambako kwamba maji ni tatizo hasa kipindi cha kiangazi, kwa kutambua umuhimu wa maji ameiomba serikali kuweza kuona namna ya kuweza kutatua changamoto hiyo kwani maji ni uhai kwa binadamu na kuna maeneo muhimu kama vile hospital na shuleni bila maji ni hatari. 

Lakini pia ameweza kugusia swala zima la Barabara katika mkoa wa Njombe, ameiomba serikali kuweza kuhakikisha inaweza kutengeneza kwa kiwango cha lami barabara zinazounganisha wilaya kwa wilaya na mkoa mwingine zilizokatika hali ya kiwango cha vumbi akitolea mfano barabara za lupembe kwenda morogoro, Njombe to Makete na wanging'ombe kwenda mbeya, amesema ili maendeleo ya maeneo hayo yaweze kupatikana kwa haraka ni lazima miundombinu ya barabara ikae sawa kwani ni mkoa inaotegemewa Sana hasa kuzalisha chakula na kusafirisha kwenda mikoa mingine hivyo serikali inawajibu wa kutatua changamoto hiyo. 

Ahsante Mbunge wetu  tunakupongeza sana kwa uhodari wa kuthubutu kuikumbusha serikali juu ya changamoto hizo. 

Imepewa Nguvu na ofisi ya siasa na uenezi mkoa wa Njombe... Shikamoo parachichi amehakikisha tumesafiri mpaka bungeni kukuletea habari hii..

Maoni