MBUNGE WA VITI MAALUM KUTOKA MKOA WA NJOMBE AIPONGEZA SERIKALI YA JPM KWA KUIMARISHA HUDUMA ZA MATIBABU YA KIBINGWA.

Na Stambulititho,  Njombe. 

Mbunge wa Viti Maalum toka Mkoa wa Njombe Mhe.Neema Mgaya ameipongeza na kuikumbusha Serikali kuwahudumia wananchi wake.

Akichangia hoja bungeni katika Wizara ya Afya, Mhe.Mgaya alianza kwa kumpongeza Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli na Serikali ya Ccm kwa kuweza kuimalisha matibabu ya kibingwa ya kupandikiza Figo na upatikanaji wa Vifaa na upandikizaji wa Vifaa vya Usikivu,ameishukuru Wizara ya Afya kwa kuhakikisha huduma zinapatikana kwa gharama nafuu na kwa wakati.

Pia Mhe.Mgaya ameishukuru serikali kwa kutimiza moja ya mapendekezo yake ya Budget mwaka 2017/18 aliposhauri Serikali kutenga budget ya kinga ya saratani ya shingo ya kizazi na serikali imeweza kufanya hivyo na wasichana wameanza kupata chanjo hiyo.

Lakini pia ameiomba serikali kuweza kuwekeza katika swala zima la utoaji elimu kwa jamii juu ya swala zima la Afya.  

Na alimtaka Waziri kujibu hoja ni kiasi gani kimepangwa ili kumaliza ujenzi wa Hospital ya mkoa wa Njombe ili ianze kutumika. 

"Serikali ilitupa pesa za ujenzi wa hospital ya rufaa mkoa wa Njombe na bado haijakamilika, namuomba mheshimiwa Waziri aseme ni kiasi gani kimepangwa ili kumaliza ujenzi na ianze kutumika" alisema Mhe.Mgaya. 

Ameweza pia kupongeza juhudi za serikali na wadau juu ya upambanaji wa maambukizi ya UKIMWI mkoani Njombe,kwani dalili njema zimeanza kuonekana kutokana na kupungua kwa takwimu za maambukizi ya Ukimwi mkoani umo kwa asilimia kubwa,na kuishauri serikali kuwa mbinu shirikishi itumike kwa wananchi ili  kuepusha kupoteza nguvu kazi ya taifa

Mwisho amehitimisha kwa  kuishukuru serikali kwa upatikanaji wa Dawa za TB kwa watoto na jamii nzima wa ujumla,kwani ilikuwa ni changamoto,pia alitoa shukurani za dhati kwa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kwa kutoa matibabu ya moyo imekuwa ni mkombozi sasa kwa wangojwa wa moyo hapa nchini.

Maoni