MD KAYAMBO -SIWEZI KUKAA KWENYE AC OFISINI WAKATI WANANCH WANGU WANAPATA SHIDA

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg.John Lipesi Kayombo jana Ijumaa 13/4/2018 amefanya mkutano na wananchi, wafanyabiashara na wamiliki wa vibanda wa soko la Sinza Makaburini na kurejesha vibanda vya biashara 204 vilivyopo katika soko hilo chini ya umiliki wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

"Mimi ni wa tofauti, siwezi kukaa kwenye ma AC yale ofisini wakati wananchi wangu wanapata shida na wana kero nyingi, lazima nitembee ili nijionee mwenyewe na hatimaye kuzitatua ndio maana hizi mvua haziwezi kuzuia mimi na wataalamu wangu kuendelea na ziara, tutazunguka pamoja na tutalowa pamoja" alisema MD KAYOMBO.

#UBUNGO YA TOFAUTI.

#HAPA KAZI TU.

Maoni