Mgogoro wa Syria,Rais wa Marekani afikiria kuyaondoa majeshi yake nchini humo.

Screen Shot 2018-04-04 at 12.08.05 PM

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema anafikiria kuyaondoa majeshi ya Marekani nchini Syria na atatoa uamuzi hivi karibuni kuhusu kupunguza msaada nchini humo.

Akizungumza jana na waandishi habari pamoja na viongozi wa mataifa ya Baltic, Rais Trump amesema lengo hasa la majeshi ya Marekani lilikuwa kuwatokomeza wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS na kwamba wanakaribia kuikamilisha kazi hiyo.

Amesema anataka kuwarejesha wanajeshi nyumbani ili kulijenga taifa lao huku akisema kuwa Marekani imetumia Dola trilioni 7 katika Mashariki ya Kati kwa miaka kadhaa na haijanunua chochote zaidi ya vifo na uharibifu.

Maoni