MHE. VULLU ASHUSHA NEEMA KWA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM PWANI.

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Mhe. Zaynabu Vullu ametoa msaada wa Bendera na Kadi za CCM zenye thamani ya zaidi ya Shillingi Million Mbili na Laki Tatu kwa lengo la kukiimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani. 

Katika Msaada huo Mhe. Vullu amekabidhi Bendera 30 na Kadi 500 za CCM ambapo pia ameahidi kutoa Bendera nyingine 30 na Kadi 500 kwa kila Wilaya za Mkoa huo.
Akikabidhi msaada huo kwa mwenyekiti wa UWT Pwani, Mhe. Vullu amesema vifaa hivyo vitasaidia kuongeza idadi kubwa ya wanachama wapya kuenda sambamba na Mkakati wa UWT Taifa kwakuwa Chama cha Mapinduzi ndicho chama kinachokubwalika na Watanzania. 

Aidha Mhe. Vullu ametumia hafla hiyo kuwahimiza kinamama kubuni miradi ya maendeleo kwa kuanzisha viwanda vidogovidogo ili kuunga mkono kaulimbiu ya serikali ya Rais Dr. John Magufuli inayohimiza Uchumi wa Viwanda. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha Mjini Bi.Judith Edward amemshukuru Mhe.Vullu kwa kuwapatia msaada huo ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya wanachama ndani ya jumuiya na Chama cha Mapinduzi. 

Maoni