MJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM MKOA WA MAGHARIBI ATOA MSAADA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA MILIONI MOJA NA LAKI TATU.


Mjumbe wa Baraza Kuu Uvccm Mkoa wa Magharibi Ndg.Kassim Hassan Haji leo Apr 05, 2018 atoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi Milioni Moja na laki tatu katika hospitali ya Chukwani Zanzibari.

Vifaa hivyo vilivyo pokeliwa na Doctar Halima Abdala Hamisi na kumshukuru Mjumbe huyo wa baraza kuu.

"Tunaishukuru Uvccm kwa sapoti yenu na kuona upungufu wa vifaa tiba kwenye hosptali hii tunawashukuru sana tena sana mungu awabariki sana" alisema Dr.Halima 

"Kwa hakika mmekuwa mfano wa kuigwa,mzidi kuendelea kuwa na moyo huo huo" Alisema Dr.Halima.
Sambamba na ilo Umoja wa Vijana Mkoa wa Magharibi walifanya usafi kwenye hospitali hiyo,lengo kubwa likiwa ni kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari na kuomboleza kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibari hayati Sheh Abedi Amani Karume. 

Uku sheha wa shehiya ya Chukwani Ndg.Selemani Mohamedi aliushukuru umoja wa vijana kwa kuwajali wakina mama wajawazito na watoto kwa kufanya usafi kwenye kituo hiko. 

"Hatukutegemea hili mlilokuja kulifanya leo hapa tunawashukuru na kuwapongeza kuwa na moyo wa namna hii" Alisema Sheha Seleman Mohamedi..

Maoni