MJUMBE WA BARAZA KUU UWT TAIFA (BARA) ATOA ELIMU KWA AKINA MAMA.

Mjumbe wa Baraza Kuu UWT Taifa (Bara)Dr Lucy Mwanisawa, amekutana na akina Mama wa kata ya Mbumi wilaya ya Kilosa,akiwa na Mtendaji wa kata ya Mbumi pamoja na Katibu UWT kata ya Mbumi,ametoa elimu kwa akina Mama wa kata hiyo ili kuunda vikundi na baadae kujiunga na SACCO'S ili waweze kunufaika na asilimia 5% zinazotolewa na Halimashauri ikiwa ni agizo la Mh Rais JPM kwa ajili ya kuinua uchumi wa akina Mama,sambamba na hilo Mjumbe amewaasa akina Mama kuwaonya watoto wao pindi wanapoona wanakwenda kinyume na maadili ya Kitanzania,ikiwa ni pamoja na kuwakanya vijana kutumia Lugha za matusi na kuheshimu Wazazi wao majirani na hata viongozi pamoja na kutumia  mitandao ya kijamii kujifunza ubunifu au mambo yanayofanywa na wengine ya maendeleo,pia kuwakanya kujihusisha na maandamano yasiyokuwa na tija.
Pia amewaahidi kuwaletea wataalamu watakao toa elimu juu ya ujasiliamali na kilimo cha biashara mfano Kilimo cha mikorosho ili kutimiza ilani ya CCM ya kuelekea uchumi wa Viwanda,na mwisho kabisa Mjumbe amewaambia akina Mama kujinenea mema na kila siku waseme "Tunaweza".na wachape kazi kwa bidii bila kukata Tamaa.

Maoni