MKALIPA AMUUNGA MKONO MH.PAUL MAKONDA

Jumapili 1 April 2018.

Na Shabani Rapwi.

Chamazi,  Dar es Salaam. 

Katika kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda juu ya kuanzisha mashindano ya club za jogging Mkoa wa Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi Ndg. Nasri Mkalipa amefanya shindano la kukimbia kwa vijana wa jogging 12 zilizopo Katika Kata hiyo. 

Mashindano hayo yaliyohusisha mbio za mita 400 na yaliyopewa jina la MKALIPA  PASAKA HALF MARATHON yamefanyika leo katika uwanja wa Mpira wa Miguu wa shule ya Msingi Chamazi.

Mshindi katika mashindano hayo yaliyoratibiwa na Katibu hamasa na Chipukizi wa Kata hiyo Ndg.Najim Nyanza na kuhusisha jogging za Shinning Star,Rufu, Vijana kombaini (Kwa Mkongo), Sound Track, Kisewe, Kiponza, Msufini, Convoy, Black Stone,Mzambarauni na Ocean ni mkimbiaji wa jogging ya Ocean kutoka katika Tawi la UVCCM DOVYA B Ndg.Twaha Shabani. 

Akizungumza kabla ya kuanza mbio hizo za mita 400 Ndg.MKALIPA aliwataka Vijana wa Kata hiyo kushiriki katika michezo mbalimbali kwani ni chanzo kikubwa cha ajira.

"Katika kuhakikisha vijana wa jogging za Mkoa wa Dar es Salaam wananufaika na jogging zao, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Paul Makonda ameandaa Mashindano kwa jogging hongera sana kwake" alisema Mkalipa.

"Katika kumuunga mkono Mh.Makonda nimeamua nifanye shindano hili kwa ngazi ya Kata ili vijana na jogging zenu mjiandae kwa ajili ya ushiriki wa mashindano hayo" alisema Mkalipa na kuendelea.

"Mwisho niseme viongozi wa Chama Cha Mapinduzi tunawapenda na kuwajali vijana wa dini, kabila, jinsia na rika zote" alisema Mkalipa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa kazi za kutangaza utalii mnamo tarehe 17/3/2018 Mh. Makonda alisema Vijana wengi wa 'Jogging Club' hizo wanafanya mazoezi asubuhi halafu hawana kazi za kufanya wanarudi vijiweni, hiyo salama maana unaweza ukashangaa wakajikuta wameanza kuwa na 'speed' kubwa na matokeo yake wakapita na mikoba ya wakina mama kama hawana kazi za kufanya. Kwa hiyo sisi tunaratibu na kupitia hadhara hii niwaambie wananchi kwamba tunapanga mipango kwa kila mwisho wa mwezi kuwepo na mashindano 'Jogging Club'.

Hivyo kwa kuzingatia  alilolisema Mh.Makonda Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Kata ya Chamazi Ndg.Nasri Mkalipa akaamua kulifanya shindano hilo kwa vitendo ili kuandaa vijana wa Kata ya Chamazi Kwa ajili ya mashindano hayo.

Maoni