MSHTAKIWA MWINGINE KUONGEZWA KESI YA AVEVA NA KABURU, KUSOMEWA MAELEZO YA AWALI BAADA YA UPEPELEZI KUKAMILIKA.

Baada ya kulazwa kwa muda mrefu hatimae leo Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva amefika mahakamani kuhudhuria kesi yake ya utakatishaji wa fedha inayomkabili yeye pamoja na makamu wake Godfrey Nyange ' Kaburu'. Pia Upande wa mashtaka umedai kuwa unatarajia kumuongeza mshtakiwa mmoja katika kesi hiyo.

Aveva ambaye alikuwa akiugua na kulazwa kwa muda mrefu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, leo amefika mahakamani akiwa anatembea kwa shida huku akiwa ameshikiliwa mkono na mshtakiwa mwenzake Kaburu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, wakili wa Serikali kutoka Takukuru Leornad Swai amedai kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali baada ya upelelezi kukamilika.

Hata hivyo, wakili Swai ameiomba mahakama  ahirisho fupi kwa kuwa wanatarajia kufanyia mabadiliko hati ya mashtaka kwa kuongeza mshtakiwa mmoja.Kufuatia ombi hilo, kesi imeahirishwa hadi Aprili 12 mwaka huu kwa ajili ya upande wa mashtaka kufanya mabadiliko hayo na washtakiwa kusomewa Maelezo ya awali.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na Mashtaka matano ya uhujumu uchumi ikiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na utakatishaji ea fedha ambazo ni Dola za Marekani (USD) 300,000.

Baada ya kuugua kwa muda mrefu hatimae leo Rais  wa klabu ya Simba, Evans Aveva amefika katika mahakamani, pichani akitoka mahakamani baada ya kesi yake inayomkabili yeye na makamu wake Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu kuahirishwa hadi Aprili 12, mwaka Huu.

Maoni