MSTAHIKI MEYA MWITA AWATAKA VIONGOZI SERIKALI ZA MITAA KUEPUKA KUWAUZIA WATU MAENEO YA MABONDENI

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Isaya Mwita

Imeelezwa kuwa changamoto ya watu kuishi maeneo ya mabondeni inatokana na baadhi ya viongozi wakiwemo wa serikali za mitaa kusimamia uuzaji wa viwanja kinyume na sheria inavyotaka.

Hayo yameelezwa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Isaya Mwita wakati akizungumza na kipindi hiki kufuatia changamoto ya mvua zinazoendelea kunyeesha jijini hapa ambazozimekuwa zikiwaathiri wakazi wa maeneo hayo.

Mstahiki Meya Mwita amesema ni vyema watu wakaondoka kwenye mabonde ili kuepuka kuhatarisha maisha yao kwani wao ndio nguvu kazi ya taifa.

Ameeleza changamoto zinazoikumba jiji la Dar es salaam kuwa ni pamoja na kutokuwepo na mipango mathubuti ya miundombinu lakini na kusema kuwa viongozi ndio wanaopaswa kulaumiwa kwani hakuna mtu atakayeweza kujenga mabondeni pasipo kupata ridhaa ya viongozi hao.

Halikadhalika nimezungumza na Mwenyekiti wa pugu steshen Sifa Makakala ili aweze kuzungumzia kuhusiana na  suala hilo ambapo amesema huo ni utashi wa baadhi ya watu hali ambayo zio nzuri.

Hata hivyo Mstahiki Meya Mwita amewataka wananchi wa jijini Dar es salaam kuendelea kuchukua tahadhari wakati huu wa mvua  za masika zinazoendelea kunyesha ili kuepuka maafa.

Maoni