WAVUVI MTERA WAPEWA ONYO, KUPITIA KIFO CHA MTOTO ALIEFARIKI AKICHEZEA MTUMBWI BWAWANI.

Wavuvi  wa samaki waliopo kandokando ya bwawa la Mtera wameonywa kutowaachia watoto kutumia mitubwi kutokana na madhara yanayopelekea   kuhatarisha maisha yao.


Wito huo umetolewa na Diwani wa kata ya mtera BW,AMONI KODI mapema leo kufuatia tukio la hivi karibuni ambalo limesababisha kifo cha mtoto mmoja aliyepoteza maisha,baada mtubwi aliokuwa akichezea kupinduka ndani ya bwawa hilo.

Akizungumza kuelekea  ziara na wakazi wa vijiji vya Chibwegere na mtera  wanaojishughulisha na uvivi wa samaki,amesema lengo la ziara hiyo ni  kutoa elimu kwa wavuvi hao kuweka walinzi ili kudhibiti watoto kuchezea vyombo hivyo vya uvuvi.

BW,KODI ameongeza  kuwa wazazi wanatakiwa kuwalinda watoto wao pamoja na kutowaruhusu kuchezea mitumbwi hiyo na amewasihi wakazi hao waliopo kandokando ya bwawa kuhakikisha wanaweka walinzi makini watakaosaidia  ulinzi wa watoto.

Hata hivyo amesema kuwa mbali na madhara ya kuachwa kwa mitubwi hiyo,pia hatari nyingine inayoweza kutokea  ni pamoja na kushambuliwa na viboko ambao wamekuwa wengi ndani ya bwawa hilo la Mtera.

Na Mhindi Josephat.
Picha na IPPMEDIA.

Maoni