MWANAMKE JITAMBUE,IJUE THAMANI YAKO - VERONICA MOSES

Aliyekuwa Mgombea Baraza Kuu UVCCM Taifa Ndg.Veronica Moses leo April 10,2018  amewataka watoto wakike kujitambua na kujua thamani ya  usichana wao wasikubali kutumia usichana wao vibaya kwa kushawishiwa ama kwa tamaa za siku moja kwani majuto yake yanakuwa maisha,uku akiwataka baadhi ya wanaume wenye tabia ya kuwatelekeza wanawake na kukimbia wanapaswa kufahamu na kutambua na heshima ya mwanamke kwani bila mwanamke akuna mwanaume na bila mwanaume akuna mwanamke,hayameyasema hayo wakati alipo kuwa kwenye hafla fupi ilio fanyika kwenye Tawi la Tanesco Kata ya Saranga wilaya ya Ubungo.

"Wanawake ni kitu muhimu sana katika hii Dunia, Mwanamke ni Jasiri Napenda kuwaomba na kuwahasa wanawake wenzangu, Msikubali kuzalishwa tu na kuachwa" alisema Veronica

"Mwanaume anakuja anakwambia anakupenda muda mfupi tu anaomba Mtoto usikubali kuwa mjinga Mwambie hivi Nioe kwanza niwe mkeo" alisema Veronica

"Kuna baadhi ya wanawake wenzetu wanapenda kujirahisha kwa wanaume nawaomba acheni hiyo tabia,mwisho wa kujirahisisha ni Mimba na mwanaume anakwambia sikutaki"  alisema Veronica

Sambamba na hilo Ndg.Veronica amewataka wanawake kujifunza kuwaepuka wanaume wasio kuwa na malengo pia amewataka wanawake kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es salamu Mh.Paul Makonda kwa juhudi na upendo wa dhati wa kuthamini wanawake.

"Nawaomba wanawake wote tumuunge mkono Mh.Paul Makonda pia tumpe ongera na Tuungane kwa pamoja wanawake wenzangu ili tukomeze hili janga kwani tumekuwa tunadharauliwa sana sababu tunajiachia achia tu Unakuta msichana ana watoto 5 na kila mmoja ana baba yake na hajaolewa sasa jiulize" alisema Veronica

"Msichana mwenzangu usikubali kuwa chombo cha kuzaa na kukimbiwa, Mwanamke Simama Imara We Ni jeshi Kubwa Ujitambue" alisema Veronica

"Niwaombe wanaume wanaotambua thamani zetu watusaidie kukombo hili janga na mungane na Mkuu wa Mkoa Mh.Makonda kutokomeza utelekezaji" alisema Veronica

Mwisho kabisa aliwaomba wanawake kujiheshimu,kujithamini,kujitunza,kujipenda na kutaka kujiona wapekee uku akiwasistizia ubunifu na kuepuka kuwa tegemezi na kuwaomba wasichana ambao bado hajazaa kujitunza na kujiheshimu..

Maoni