MWENYEKITI UVCCM WILAYA YA RUFIJI, AWASHA MOTO RUFIJI HAIJAWAI KUTOKEA

Mwenyekiti uvccm wilaya ya RUFIJI Ndg.Juma Seif Kwangaya leo Aprili 15,2018 amezindua michezo kwa vijana wa tarafa ya ikwilili.

Michezo amabayo mwenyekiti ameizindua ni Football, Rede na Jogging kwa kugawa vifaa vya michezo kwa vijana hao. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Ndg.Kwangaya amewataka vijana kujitokeza kwa wingine kwenye michezo na kuifanya michezo kuwa chanzo cha ajira kwao. 

"vijana msiwe nyuma kwenye michezo kwani michezo sasaivi ni chanzo cha ajira, mifano mingi ipo ya watu walio fanikiwa kwenye michezo kama vile Bwana Samatta,  Msuva na n.k ivyo niwaombe muitumie michezo Kama chanzo cha ajira na kuja kunufaisha nyinyi wenyewe na kuwa na maisha mazuri na kuupa sifa mkoa wetu wa pwani" alisema Kwangaya 

"Uwezi kufanikiwa kwenye michezo kama utakuwa na nidham mbovu ivyo mzingatie nidhamu kumuheshimu mkubwa na mdogo pia jiamini kwenye kile unacho kifanya rakini usije kumsahau Mungu, mtangulize Mungu mbele kwenye kila jambo" alisema Kwangaya

 

Mbali na kuzindua michezo hiyo, vijana walipata fursa ya kupata elimu kutoka kwa Afisa maendeleo ya Jamii ili kuweza kujiinua kiuchumi. 

Nae Afisa maendeleo ya vijana amewaambia vijana kupata 4% ni lazima na ni haki yako kishelia ila ni lazima vigezo vifuate ili waweze kupata pesa hizo.

Washiriki wakuu wa michezo hiyo ni chuo cha ufundi stadi (FDC), kata ya mgomba, kata ya umwe na kata ya ikwilili kati. 

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Mjumbe wa baraza kuu Uvccm wa Pwani Ndg. Hamza kiuta Afisa maendeleo ya Jamii Ndg.Nasri  Mwalimu mkuu wa chuo cha ufundi stadi. 

Maoni