Mwenyekiti wa kijiji cha kilombero 1 jela miaka mitatu.


GEITA Mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Geita imemhukumu Mwenyekiti wa kijiji cha Kilombero 1 Bw. Mahano Bitendo Bihogo (Pichani) kwenda jela miaka mitatu kutokana na kukutwa na hatia ya makosa matatu ambayo ni kushawishi na kupokea hongo kinyume na kifungu cha 15(1)(a)na(2)cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu cha sheria na kanuni za adhabu sura ya 16 R:E 2002 Katika shauri la jinai Na.114/2018
.
.
Akisoma hukumu hiyo mbele ya mwendesha mashitaka wa Takukuru Bw. Kelvin Murusuri Hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Geita, Kaliho Mrisho amesema mahakama imemkuta na hatia mshitakiwa na kwamba mahakama imejiridhisha pasipokuwa na shaka yoyote na ushahidi ulioelezwa na mwendesha mashitaka Bw. Murusuri baada ya mtuhumiwa kukiri kutenda makosa hayo

Maoni