MBUNGE VITI MAALUM MHE.NEEMA MGAYA AIOMBA SERIKALI KUZITATUA KERO ZA WANANCHI WA MKOA NJOMBE.

Na Titho Stambuli Mtokoma na Erasto Kizumbe 

Mtu kwao ni msemo Tuuuu

lakini kwa  Mbunge wa viti maalumu Neema Mgaya kutoka mkoa wa Njombe ameutafsiri kwa vitendo zaidi Bungeni.
 
Mbunge machachari kutoka mkoa wa Njombe, ameonekana kupasua anga na kulitikisa bunge pindi achangiapo hoja bungeni ameonekana kuichambua Njombe kila kona na kuikumbusha serikali wapi haijatimiza wajibu wake kwa wapiga kura wake.

Ukiachana na uhodari na uwezo wa Mbunge huyo, ameonekana kuzidi kuwakumbuka wananjombe pindi apatapo nafasi ya kuchangia hoja bungeni. 

Ni Mh Neema Mgaya tena pale alipopata nafasi ya kupaza sauti wakati wa kuchangia hoja katika wizara ya TAMISEMI, kwa upande wake bado begi Lake limejaa kero za Njombe na kwa kutambua kuwa amechaguliwa kwaajili ya kuiletea Njombe maendeleo, ameweza kuikumbusha serikali kutatua kero zifuatazo mkoani Njombe.

Kero ya kwanza ameipa kipaumbele sekta ya elimu kwa kuiomba serikali kuwaajili walimu wa sayansi katika shule za sekondari kwani wamekuwa ni wachache na kushindwa kufanikisha malengo ya wanafunzi mkoani Njombe, lakini pia ameiomba serikali kuweza kuwaajili walimu wa shule ya msingi mkoani Njombe kwani waliopo hawatoshi na hawawezi kumudu idadi ya wanafunzi waliopo mashuleni. 

Pia ameiomba serikali kutoa kibali cha kuweza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano kwa shule za sekondari makoga, wanike na manda kwani tayari wananchi kwa kushirikiana na halmashauri wameweza kuboresha miundo mbinu ya shule hizo na hivyo kuwa na sifa zote.

Pia Nguli Huyo siasa bado anakumbuka afya ndio kila kitu ameiomba serikali kuweza kuongeza wataalamu wa afya mkoani Njombe, kujenga hospital ya Wilaya Wanging'ombe na Njombe DC na kujengewa jengo la upasuaji na miundo mbinu yake kituo cha afya Makoga na ambulance kwani wananchi wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo,pia kwa upande wa Ludewa ameiomba serikali kuongeza nguvu kwa wananchi na ambao wako tayari kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wanajenga vituo vya afya kwa kuhakikisha swala la afya kwa wanachi wake linakuwa sawa. 

Lakini pia ameitahadharisha serikali ili uchumi wa Njombe ukue haraka miundo mbinu bado ni kiungo muhimu, ameiomba serikali kujenga daraja la ilembula linalo unganisha makao makuu ya Wilaya ambapo wananchi wamekuwa wakifika huko kwaajili ya kupata huduma za kijamii na biashara na kwa upande wa ludewa ameweza kuiongelea barabara ya Lupingu kwenda matema Beach, amesema barabara hii ni muhimu sana kwani shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii zinakwama kutoka na kutokuwa na barabara nzuri inayowawezesha wananchi kufanya shughuli zao kwa ufanisi Mkubwa .

Amewakumbuka pia wanawake na vijana ameiomba serikali kufuatilia Kwa ukaribu zaidi swala la mikopo kwa makundi hayo kwa kuhakikisha wakurugenzi wanawajibika kadri ya makubaliano ili kuweza kusaidia kuboresha maisha ya makundi hayo, ameonekana akiongea kwa msisitizo zaidi kwani yeye pia ni kijana na ni Mwanamke hivyo anakila sababu ya kuyapigania makundi hayo. 

Tunakupongeza mbunge wetu kwa kutimiza wajibu wako. 

Maoni