NDEGE ZINA FAIDA GANI KWA MTANZANIA

Na Emmanuel J. Shilatu

Tangu Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli iingie madarakani imekazania kununua ndege kwa ajili ya Shirika la ndege la Tanzania (ATCL). Baadhi ya Watu wanahoji kwanini pesa hizo za kununulia ndege aina ya Bombardier Q400 zisingeelekezwa kwenye shughuli zingine za kimaendeleo? 

Ndege zina faida gani kwa Mtanzania?

1. Ndege inaokoa muda; Safari ya basi, meli ama treni ambayo ungetumia siku nzima ama siku mbili kwa ndege unatumia dakika kadhaa kufika. Ndege inaokoa rasilimali muda kwa kusafirisha Watu na mizigo.

2. Ndege inatoa fursa za ajira; kupitia usafiri wa ndege inatoa fursa za ajira kwa wahudumu wa ndege, manahodha, wabeba mizigo, waongoza ndege, wakata tiketi, mafundi nk. Hivyo kupitia ndege inapunguza tatizo la ajira nchini kwa kuimarisha mapato binafsi ya Watu na kusaidia kuendesha familia zao na wategemezi wao.

3. Kufufuka kwa shirika la ndege; hakuna asiyejua shirika letu la ndege la ATCL lilikuwa kwenye hali mbaya, ununuaji wa ndege mpya unaleta uhai na ufufuo wa shirika la ndege linaloleta ushindani na uboreshwaji wa huduma za ndege nchini, inaleta heshima mpya kwa shirika kitaifa na kimataifa. 

4. Inaongeza mapato ya nchi; kupitia makusanyo ya mauzo ya tiketi, kodi inayokatwa kwenye tiketi Serikali inaongeza kiasi cha makusanyo ya ndani ya nchi. Makusanyo hayo ndio huelekezwa kwenye huduma za kijamii, ujenzi wa miundo mbinu, kutoa elimu bure, kutoa huduma za kiafya n.k

5. Inasaidia shughuli za kibiashara; ndege inasaidia kusafirisha Watu na mizigo kwa Wafanyabiashara kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kwa haraka zaidi. Shughuli za kibiashara zinaporahisika zinasaidia mapato na uchumi wa nchi kuongezeka na kuimarika zaidi.

Mtu aliyepo kijijini anafaidikaje na hizi ndege?

1. Kupitia makusanyo yanayopatikana, Serikali inapata uwezo wa kuwahudumia Wananchi wake wakiwemo waliopo vijijini kwa kuwapeleka huduma za kiafya, nishati ya umeme, maji pembejeo za kilimo, ujenzi wa barabara, madaraja na vivuko n.k.

2. Wale wanaoajiriwa kwenye ndege husaidia kutoa huduma kwa familia zao, ukoo na Wategemezi wao wakiwemo waliopo vijijini.

3. Husaidia uokozi wa muda wa usafirishaji wa Watu na mizigo yakiwemo mazao ya Wakulima na hivyo kuimarisho mapato binafsi ya Watu (wakiwemo wa Vijijini) na Taifa.

Watanzania tunaelewa ndege zina faida kwa kila Mtanzania; Watanzania tunathamini na kutambua mchango mkubwa wa Serikali katika ununuaji wa ndege na ufufuaji wa shirika la ndege la ATCL.

Daima tunaunga mkono ununuaji wa ndege hizi; Daima tutasimama na Rais Magufuli

Maoni