PROF KABUDI ATAJA HATUA INAZOCHUKUA SERIKALI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA.

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesisitiza  Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na hatua  za kuhakikisha kunakuwepo mazingira wezeshaji yatayofanikisha ujenzi wa viwanda nchini. 

Prof.Kabudi amesema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya utafiti iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya REPOA ambapo mada kuu ilikuwa kujadili kuelekea jamii inayoendeleza viwanda 2025 : kwanini ushindani ni muhimu.

Pia kwenye warsha hiyo wadau wamejadili masuala ya kisera katika safari ya Tanzania kuelekea kwenye uchumi mseto na shindani ,ukiongozwa na viwanda , pamoja na kufikia nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama inavyotarajiwa kwenye dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

akizungumza  baada ya ufunguzi wa washa hiyo Profesa Kabudi ametaja hatua mbalimbali ambazo Serikali inachukua katika kufanikisha ujenzi wa viwanda nchini na kufafanua kinachoendelea ni kuangalia jinsi gani kufanya bidhaa za Tanzania kuwa na ushindani kwenye soko la Dunia.

"Kuna mambo mengi ya kufanya katika kufanikisha ujenzi wa viwanda nchini .Nikumbushe tu wakati tunapata uhuru tulikuwa na viwanda viwili , hivyo jukumu la wakati ule ikawa ni kuanza kujenga viwanda na vilijengwa na kutoa ajira kwa wananchi.

"Hata hivyo ilipofika mwaka 1977 baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki tukarudi nyuma kidogo na baadae tukaingia kwenye vita dhidi ya Uganda ambapo tulitumia dola za Marekani milioni 5 kwenye vita.Hivyo tukawa hatuna fedha za kuendeleza viwanda.

"Pamoja na magumu ambayo tumeyapitia bado leo hii tunavyo viwanda vingi ingawa jukumu la Serikali ni kujenga viwanda zaidi ili kuboresha maisha ya wananchi wake katika kuleta maendeleo,"amesema Profesa Kabudi.

 Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi akizungumza na wadau wa utafiti wakati akifungua Warsha ya siku mbili kwa watafiti wa Tanzania na kutoka nje iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya REPOA jana jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi  Amina Salim Alli akizungumza wakati anaongoza mjadala juu ya Uchumi wa Viwanda kufikia 2025

 Mtoa mada Mkuu wa Warsha hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za kusini mwa Afrika katika mausuala ya forodha(SACU), Paulina Mbala Elago akitoa mada yake juu kwanini Ushindani na jinsi ya kuufikia katika maendeleo ya viwanda katika nchi hizo.

 Mkurugenzi Mkuuu wa Tasisi  ya utafiti nchini Repoa Dk Donald Mmari akizungumza kabla ya kumkaribisha msemaji mkuu katika warsha hiyo ya kwanini ushindani juu ya viwanda kufikia 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Infotech Investment Group LTD , Ali Mufuruki akiongoza majadiliano ya hali ya biashara kwa sasa katika Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Repoa nchini.

 Baadhi ya Washiriki waliohudhuria Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Tasisi ya Utafiti nchini Repoa wakifuatilia mijadala mbalimbali

  Baadhi ya Washiriki waliohudhuria Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Tasisi ya Utafiti nchini Repoa wakifuatilia mijadala mbalimbali.

Maoni