Rais Magufuli alezea jinsi alivyopokea taarifa za kifo cha Sokoine.

Leo April 12, ni kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Moringe Sokoine ambaye alifariki kwa ajali ya gari akitoka Dodoma katika vikao. Rais Magufuli ameeleza jinsi alivyopokea taarifa za kifo cha Sokoine na mengine.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter JPM ameandika

“Katika siku kama ya leo tarehe 12 Aprili 1984 nikiwa Mpwapwa JKT nikitumikia jeshi langu “Oparesheni Nguvukazi” tukatangaziwa kifo cha marehem Edward Moringe Sokoine, ilikuwa siku ya majonzi shujaa huyu niliyemjua na kumshabikia ikawa siku yake ya mwisho.”

“Wakati tunapoazimisha siku kama hii ya kifo chake, watanzania tuige mfano wake kwani alikuwa msema kweli, asiyeogopa, mpiga vita rushwa,ufisadi, unyonyaji,mzalendo wa kweli na aliyechukia rasilimali za watanzania kuibwa” -Rais Magufuli
“Marehem Sokoine hatasahaulika katika historia ya Tanzania, ni wito wangu kwa watanzania tumuige na kumuishi. Ni rai yangu pia tumuenzi kwa kujenga umoja wetu , kupiga vita rushwa na kuchapa kazi . Mungu aiweke roho ya marehemu Edward Moringe Sokoine mahala pema peponi” -Rais Magufuli

Maoni