SERIKALI YAWAREJESHA KAZINI WATUMISHI WA DARASA LA SABA


Serikali yatangaza kuwarejesha kazini watumishi 1,370 wenye elimu ya darasa la 7 walioondolewa kwenye ajira kwa kukosa sifa ya kuwa na elimu ya kidato cha nne.
-
Watumishi wote watalipwa mishahara yao yote tangu walipoondolewa katika mfumo ajira
-
Aidha, Serikali imeagiza kuwa Watumishi(Watendaji wa Vijiji na Mitaa) wote walioanza kazi kabla ya Mei 20, 2004 ulipoanza kutumika waraka wa utumishi warejeshwe mara moja
-
Uamuzi huu wa kuwarejesha watumishi hawa hautawahusu, waliowasilisha vyeti vya kughushi na taarifa nyingine za uongo
-
Watendaji na Wakuu wa Idara waliohusika kuwaajiri watu wasiokuwa na sifa baada ya Mei 20, 2004 watachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.

Maoni