Shambulizi la kijitoa muhanga Afghanistan,Idadi ya waliouawa wafikia 31 huku wengine zaidi ya 50 wakiripotiwa kujeruhiwa.

Idadi ya watu waliouawa katika shambulizi la kujitoa muhanga kwenye kituo cha ugawaji wa vitambulisho vya taifa hii leo mjini Kabul imepanda na kufikia watu 31.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya Afya ya Afghanistan kiasi ya watu 56 waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali zilizoko kwenye mji huo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani amesema mshambuliaji aliyekuwa akitembea kwa miguu alijtoa muhanga baada ya kulipua vesti ya miripuko aliyokuwa amevalia nje ya ofisi ya kugawa vitambulisho vya taifa katika eneo linalokaliwa zaidi na washia mjini Kabul.

Kituo hicho ni maalumu kwa ajili ya kugawa vitambulisho vya taifa kwa wapiga kura kabla ya uchaguzi wa bunge na mabaraza ya majimbo uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Kundi la itikadi kali linalojiita Dola la Kiislamu limedai kuhusika na shambulizi hilo.

Maoni