SPIKA NDUGAI APIGA MARUFUKU UKAGUZI WA KUWASHIKA SHIKA WABUNGE

 Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ameagiza kusitishwa mara moja ukaguzi wa kuwashika shika wabunge mwilini na kuagiza utaratibu mpya ufanyike kwa kuangalia namna bora ya kuwakagua wabunge.

Kauli hiyo ilitolewa na spika bungeni Dodoma wakati akitoa mwongozo alioombwa na Mbunge wa Kavuu (CCM), Pudenciana Kikwembe, ambapo alimwomba mhe.Spika kupiga marufuku ukaguzi wa aina hiyo na kudai kuwa ukagizi huo ni uzalilishaji.

Kikwembe alisema wanapopita kwenye mashine za ukaguzi hutakiwa kuvua mikanda, viatu, saa na vitu vingine na kwamba kibaya zaidi kwake ni suala la kupapaswa.

“Tunavua nguo, watu wanainua mashati kuvua mikanda na tunaona vitovu vya wanaume halafu miili inasisimka wa binadamu una vivutio vingi”

“Leo nimepita mashine moja vizuri na nilipofika ya pili ikalia. Nikaambiwa nikaguliwe sasa kibaya nakwenda kukaguliwa ananishikashika maeneo mbalimbali” alisema Kikwembe.

Maoni