Tuzo za Sinema Zetu: Gabo Anyakua Tano, Wema Sepetu Mbili Waacha Historia

Usiku kuamkia  leo katika ukumbi wa Mlimani City macho ya Watanzania yamepata kushuhudia zoezi la ugawaji wa tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF) zenye jumla ya vipengele 18 huku kimoja kikiwa cha People Choice na kukamilisha vipengele 19 ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Mstaafu wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni mualikwa akiwa muigizaji kutoka India aitwaye Pritika Rao maarufu kama Aliyah ambaye amejizolea umaarufu kupitia tamthilia ya ‘Beitehaa’.

Katika usiki huo uliopambwa na muziki tofauti kutoka ndani ya Tanzania, mastaa mbalimbali katika sekta ya burudani wamepata kushuduhia tuzo hizo zilizoweka na kuandika historia kwa wasanii kama vile Gabo Zigamba aliyenyakuwa jumla ya tuzo tano huku malkia wa filamu nchini Wema Sepetu aliondoka na tuzo mbili na filamu ya ‘Binti Zanibar’ ikiondoka na tuzo.
wema sepetu akiwashukuru watanzania kwa kumpenda na kuifanya filamu yake ya Heaver Sent kushinda tuzo ya Chaguo la Watazamaji,kati ya filamu zaidi ya 140 ziizooneshwa.
GaboZigamba akitoa shurani zake baada ya kutwaa tuzo ya muigizaji bora wa kiume.

Maoni