VIJANA WA CCM MPANDA WAONYWA.


Vijana wa Chama cha Mapinduzi ccm wilayani Mpanda wameonywa kutoingiza masuala ya udini na ukabila kwenye siasa.

Hayo yamesemwa na katibu wa umoja wa vijana wa chama cha cha mapinduzi UVCCM Bwana Deus Thomas katika mkutano na wananchi wa kata ya Kanoge.

Bwana Thomas amewataka vijana kujikita katika kutekeleza sera za chama hicho kwani ndizo zinazowaunganisha

Aidha ameongeza kuwa chama hakitasita kuwachukulia hatua kali zikiwemo kuwafuta uanachama wale wote watakaobainika kwenda kinyume na matakwa ya chama.

Maoni