WAHAMIAJI HARAMU TISA RAIA WA ETHIOPIA NA MTANZANIA MMOJA WALIVYODAKWA NA POLISI MORO.

POLISI Mkoani Morogoro inawashikilia  wahamiaji haramu tisa ambao ni wa Ethiopia na Mtanzania mmoja ambaye ni dereva aliyekuwa anawasafirisha kwa gari  lenye namba za usajili  T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili  T229 DBW ikitoka Dar es Salaam kuelekea  Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.

Kamanda wa Polisi wa  mkoa wa Morogoro , Ulrich Matei  alisema  kuwa tukio la kukamatwa kwa raia hao lilitoke Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi , mkoani Morogoro katika barabara ya Morogoro- Iringa.

Kamanda Matei alisema, raia hao  walikuwa wamepakiwa wakiwa wamefichwa katika chasis ya gari hilo  baada ya kutandazwa mbao ambalo lilikuwa  likiendshwa na  Mbaruku Kassim (40) mkazi wa Tabata  Jijini Dar es Salaam ikitkea  kutokea Jijini humo kuelekea Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.

Aliwataja raia hao wa Ethiopia waliokamatwa ni Taka Desta (24), Muluma Achiso (22), Mintensinot Workineh (23),Tesfhun Getachew (19), Muligeta Lalago (19), Zachewo Tikaso (20),Sekadu Abate (14), Asra Said (18) na Esafa Ercafo (22).

“ Raia hawa walihifadhiwa chini ya chisis ya gari baada ya kuwekwa mbao na wao kujificha eneo hili jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao ,  kitendo hiki ni kibaya “ alisema Matei.

Hata hivyo alisema , Polisi itaendelea  kufanya ukaguzi na  msako mkali  katika maeneo ya njia zote kuu za mkoa huo ili kukomesha biashara hiyo haramu na watakaokamatwa wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

 Kwa mujibu wa Kamanda wa mkoa  kuwa, watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa ili waweze kukabidhiwa kwa Idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kuwafikisha mahakamani.

 Kamanda wa Polisi Morogoro, Ulrich Matei  akitoka kukagua gari iliyokamatwa na  wahamiaji haramu tisa raia wa Ethiopia, Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi ,mkoani Morogoro wakisafirishwa kwenye  gari  lenye namba za usajili  T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili  T229 DBW iliyokuwa ikiendeshwa na Mbaruku Kassim (40) ( mwenye shati ya miraba mkazi wa Tabata  Jijini Dar es Salaam  wakitokea  Jijini humo  kuelekea  Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.

 Kamanda wa Polisi Morogoro, Ulrich Matei  akitoka kukagua gari iliyokamatwa na  wahamiaji haramu tisa raia wa Ethiopia, Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi ,mkoani Morogoro wakisafirishwa kwenye  gari  lenye namba za usajili  T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili  T229 DBW iliyokuwa ikiendeshwa na Mbaruku Kassim (40) ( mwenye shati ya miraba mkazi wa Tabata  Jijini Dar es Salaam  wakitokea  Jijini humo  kuelekea  Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.

 Kamanda wa Polisi Morogoro, Ulrich Matei  akisoma majina ya wahamiaji haramu tisa raia wa Ethiopia walikamatwa  Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi ,mkoani Morogoro wakisafirishwa kwenye  gari  lenye namba za usajili  T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili  T229 DBW iliyokuwa ikiendeshwa na Mbaruku Kassim (40) ( mwenye shati ya miraba mkazi wa Tabata  Jijini Dar es Salaam likitokea Jijini humo  kuelekea  Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.

Wahamiaji haramu  tisa raia wa Ethiopia akiwemo na Mtanzania mmoja  ambaye ni dwereva  aliyetambuliwa kwa jina la  Mbaruku Kassim (40) mkazi wa Tabata  Jijini Dar es Salaam   ( wanne kutoka kushoto) wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi baada ya kukamatwa  Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi ,mkoani Morogoro wakisafirishwa kwenye  gari  lenye namba za usajili  T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili T229 DBW  wakitokea  Jijini humo  kuelekea  Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.

( Picha na John Nditi).

Maoni