WAJASIRIAMALI WAIANGUKIA SERIKALI KUOMBA MTAJI.

Wanawake wajasiliamali wa kikundi cha Tasilija Mpadeko katika kata ya Makanyagio Manispaa ya Mpanda wameiomba serikali kuwasaidia kuwapatia mtaji katika kikundi chao kinacho jishughulisha na kazi ndogo ndogo za kujikwamua kiuchumi.

Wamebainisha hayo wakati wakizungumza na Mpanda Redio kuhusu namna ambavyo kikundi hicho kimewasaidia katika kujikwamua kiuchumi wamesema nivyema srikali ikawasaidi kuwaongezea mtaji utakao saidia kutunisha mfuko wa kikundi chao katika shughuli wanazo zifanya.

Aidha wamebainisha baadhi ya changamoto wanazo kabiliana nazo katika kikundi chao kuwa ni baadhi ya wanakikundi kutorejesha pesa kwa wakati pamoja na hali mbaya ya biashara kwa baadhi ya misimu hususani wakati wa masika.

Kikundi hicho cha Tasilija Mpadeko kina jumla ya wajasiliamali kumi na sita wanao jishughulisha na shuhguli mbali za kujikwamua kiuchumi kama vile kuchoma mandazi,kufanya bishara za kuuza mkaa na kuuza bidhaa mbali mbali sokoni.

CHANZO:Paul Mathius.

Maoni