MAKONDA UMEGUSA MOYO WANGU

Naitwa Lewis Abushiri , Mwenyeji wa Ushirombo, ila kwa sasa niko Dar es Salaam Mfanyabiashara Sokoni Kariakoo, Nina kaka yangu wa Kwanza Kuzaliwa Yeye ni Kamishna Pale TRA . 

 *Watoto Wangu wanasoma Shule Ya Msingi Ushindi, shule ambayo ina changamoto ya Uduni wa Miundombinu Haswa Madarasa na Vifaa vya kufundishia. 

 Kaka yangu ambae ni Kamishna kwa sasa alipata Bahati ya kusomeshwa Shule za Serikali kuanzia Msingi Kule Ushirombo ,Tabora Boys na kisha Chuo Kikuu Maeneo yote Alisoma BURE . 

Leo hii yeye anasomesha watoto wake Aga khan Primary Japo Hawa wanapewa Ondoleo au Punguzo la Kodi (excemption) bado Ada zao ni zaidi ya Milioni 8 kwa mwaka kwa mtoto Mmoja, Mtoto wake wa Mwisho Anasoma St Joseph Cathedral wanalipa ada 7 milioni kwa Mwaka japo pia wao kama Kanisa Wanapata Vitendea kazi vya Kufundisha wanapata exemption. 

Hoja yangu sio kumchafua kaka yangu, au kumuonea Wivu, nachotaka kusema KWANINI VITU VYA SHULE ZA WANANCHI VIWEKEWE MIZENGWE? au Labda Hawa wananchi ni wa Pagani ndio mana Wanaumia? 

Inawezekana wanaoweka MIZENGWE watoto wao wanasoma Shule Bora Kama Hizo, ila Kwangu Nakumbuka Ile Habari ya Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli alipokwenda Bandarini na kuwauliza Wahusika Kwanini Magari ya Jeshi la Polisi yako pale kwa Miaka Miwili, wakati magari yamenunuliwa na fedha za walipa kodi ambao wanahitaji Ulinzi wa Mali zao, Mbali na Mhe Magufuli kushangazwa na Hali Ile kwangu ilinifunza kitu ambacho Naomba niseme 

"BAADHI YA WATANZANIA WAKO RADHI KUHUJUMU WATANZANIA WENZAO KWA CHUKI NA HILA" 

Kwangu Mimi Makonda Amegusa Moyo wangu na wa familia yangu kwa kupambana watoto wetu wa shule za KATA wapate Elimu Bora japo ni kwa MBINDE. 

 Iweje Watanzania wazalendo Wanaoishi Ughaibuni " Diaspora *Wajichange hela zao wanazopata kwa shida na kuwasaidia wadogo zao walioko Tanzania Vifaa Bora vya kupatia Elimu , Halafu Hapo Hapo waambiwe walipie kodi vitu ambavyo wamejitolea kwa jasho Lao, Hivi tunashindwa kuwa na Busara Hata Kidogo katika Hili? 

Leo nimeshuhudia CHUKI ya kiwango cha JUU ya Baadhi ya Watu kwa Makonda. 

 Mwisho , nimalize kwa kushauri tu, Kadri Jinsi ya Baadhi ya WATU wanavyomchukia Makonda, Ndiyo hivyo hivyo MUNGU anazidi kumbariki kwa kipimo kile kile cha CHUKI , ndicho hugeuka na kuwa Kipimo cha BARAKA KWAKE.

Wasalamu 
Lewis Abushiri

Maoni