ZIARA YA MHE.ENG.HAMED MASAUNI (MB) JIMBO LA KIKWAJUNI KUANZA LEO MAY 25 MPAKA MAY 28,HIZI NDO SEHEMU ATAKAZO ZITEMBELEA WAKATI WA ZIARA.

Mhe.Eng.Hamad.M.Y.Masauni (Mb) jimbo la Kikwajuni kuanza ziara yake leo May 25 na kufikia tamati May 28,2018. 

Na hii ndo ratiba kamili ya ziara yake. 

Ijumaa, tarehe 25/05/2018:

(i) Saa 5.30 asubuhi kuwasili Bandari ya Zanzibar na kuelekea moja kwa moja kwenye kituo cha vijana cha Tanzania Youth Icon (TAYI), Mwembe Madema kwa ajili ya Sherehe za Makabidhiano ya mifuko 300 ya Saruji kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Jimbo la Kikwajuni;

(ii) Saa 8 mchana ni Makabidhiano ya vitendea kazi, pamoja kuaga rasmi Sekretariet ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa,  ambayo nilihudumu kama Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, Afisi Kuu ya CCM Kiswandui;

(iii) Saa 10 jioni vikao vya Kamati ya Ligi ya Masauni/Jazeerah Cup na Kamati ya Mashindano ya Quran ya Jimbo pamoja  na kukagua kiwanja na miundombinu yake kwa ajili ya maadalizi ya shughuli hizi mbili zinazofanyika kila mwaka wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani; na

(iv) Saa 2.30 kikao Mahsusi cha Kamati ya Maadalizi ya Futari, Mchapalo, Mahanjumati na Makulaji ya Jimbo.

Jumamosi, tarehe 26/05/2018.

(i) Saa 3 asubuhi kikao na viongozi wa Chama wa ngazi zote wa Jimbo na Jumuiya zake, Afisi ya CCM Jimbo;

(ii) Saa 6 mchana kukabidhi vifaa vya Michezo kwa timu zinazoshiriki kombe la Masauni/Jazeerah Cup na kuzungumza na wandishi wa habari:

(iii) Saa 10 jioni kutembelea wazee, wafiwa na wagonjwa pamoja na kukagua miradi ya maendeleo Jimboni (Ujenzi wa Tenki la Maji, Ujenzi wa Afisi ya Jimbo ya kisasa, Mafunzo ya ufundi na lugha ya kichina, Tayi, Kutembelea Skuli na Vyuo vinavyofanyiwa matengenezo, n.k); na

(iv) Saa 4 kamili usiku kuangalia fainali ya kombe la Ulaya kati ya Liverpool na vibonde Real Madrid.

Jumapili, tarehe 27/05/2018:*

(i) Saa 3 asubuhi kufanya mazungumzo na wakuu wa vyombo vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
waliopo Zanzibar;

(ii) Saa 10 jioni kujianda na mechi kali ya ufunguzi nikiwa kama kiungo wa kutumainiwa wa timu kali ya maveterani wa Kikwajuni; na

(iii) Saa 3 usiku uzinduzi rasmi wa Mashindano ya Mpira wa miguu (Masauni/Jazeerah Cup),  viiwanja vya Mnazi Mmoja.

Jumatatu, tarehe 28/05/2018:

(i) Saa 1.00 asubuhi kuelekea Uwanja wa Ndege kwa safari ya kurejea Dar Es salaam na Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Bunge vinavyoendelea.

Maoni