MWAKILISHI WA VIJANA MKOA WA KUSINI ATOA MSAADA WA TENDE, JUZUU, MAS HAF KWA WILAYA YA KATI PAMOJA NA WILAYA YA KUSINI UNGUJA.


Mwakilishi wa Vijana mkoa wa kusini Salh Mwinjuma ametoa msaada wa tende, juzuu na mas haf kwa wilaya ya kati pamoja na wilaya ya kusini unguja.
Wakipokea msaada huo makatibu wa wilaya zote mbili.

Walimshukuru mwakilishi huyo kwa kuwakumbuka Vijana asa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani. 
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Bi.Salha Mwinjuma amewahimiza vijana kusoma sana Qurani kipindi hiki cha ramadhani.

Pia amewahimiza viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi kutimiza majukumu yao kwa wakati na kukipigania Chama cha Mapinduzi hasa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu. 

Mwisho amemalizia kwa kuwataka vijana kuwaombea dua viongozi walio madarakani.

"Vijana waombeni dua maraisi wetu, rais wa Zanzibari pamoja na Wajamhuri ya Muungano, Mwenyekiti wa Uvccm, makamu Mwenyekiti ili waweze kuongoza na kuzidi kukitumikia Chama cha Mapinduzi kwa Moyo" 

Maoni