WAZIRI UMMY – SERIKALI IMETENGA BILION TATU (3) KWA AJILI YA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI

Dar es salaam: Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) ilizindua zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kili Challenge 2018), na kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa mwaka 2018 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini. Shughuli hii ilifanyika tarehe 4 Mei 2018 mwaka huu katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Ummy Mwalimu, aliitikia wito wa kufika Dar es salaam, katika hafla ya uzinduzi wa Kili Challenge 2018, ambapo alifanya zozezi la ugawaji wa fedha zilizokusanywa mwaka mwaka jana 2017 zilizopatikana baada ya wadau mbalimbali kupanda na kuendesha baiskeli kwa kuzunguzuka Mlima Kilimanjaro. 

Kili Challenge ni mfuko unachangia juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kutoa elimu kwa jamii kuhusu maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU). Kili Challenge ni mfuko muhimu unaoshirikiana na taasisi za nje na ndani ya nchi katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa jamii ya Kitanzania na Dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii inabaki bila kuathiriwa na VVU/UKIMWI katika miaka ijayo.

Mfuko huo pia unalenga kuisaidia Serikali kukabiliana na VVU//UKIMWI sambamba na kutoa nafasi kwa watalii wa ndani na nje kuupanda mlima Kilimanjaro. Uzinduzi huo ulishirikisha Tume ya kuthibiti UKIMWI, Tanzania TACAIDS, na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) ambapo zaidi ya shilingi bilioni moja (1) zilikusanywa katika tukio hilo. 

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu, ameitaka serikali kutumia mbinu mbalimbali na kuweka mikakati itayohakikisha fedha zinazotwengwa kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI zinatumika kwa kusudi hilo, na hivyo kuondokana na kutegemea misaada kutoka kwa wafadhili.

Mheshimiwa Ummy Mwalimu alisema fedha zilizopatikana kwenye harambee hiyo zinatakiwa zielekezwe moja kwa moja kwa wahusika na sio kutumika kama posho za vikao, huku zikionyesha jitihada zilizofanywa katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu, pia akiendelea kusema, fedha hizo zinatakiwa kuisaidia nchi katika kuzipa nguvu sekta ndogo ili kuthibiti maambukizi ya UKIMWI nchini. 

Mkurugenzi wa mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) Bw. Richard Jordison, akisoma hotuba kwenye hafla ya uzinduzi wa Kili Challenge 2018, iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es salaam mapema mwishoni wa wiki iliyopita.

Mheshimiwa waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Abel & Fernandes Communcations, Ms. Fatma Fernandes wa pili kutoka kulia, ambaye alinunua picha ya makamu wa Raisi Mheshimiwa Samia Suluhu katika mnada uliofanyika wakati wa uzinduzi wa Kili Challenge ili kukusanya fedha za kupambana na UKIMWI, jijini Dar es salaam mapema mwishoni wa wiki iliyopita.

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu, akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni mia moja (100M) kwa watoto wa kituo cha moyo wa huruma kilichopo Geita ili kusaidia mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa TACAIDS, Dkt.Leornard Maboko, Mkurugenzi wa GGM, Bw. Richard Jordison na kulia, Mkurugenzi wa kituo cha Moyo wa Huruma Sister Adalbera Mukure.

Mkurugenzi wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko akisoma hotuba kwenye hafla ya uzinduzi wa Kili Challenge, katika hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyoko jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu akishiriki katika harambe iliyofanyika kwenye uzinduzi wa Kilimanjaro Challenge ili kuchangia mfuko kwa ajili ya kudhibiti UKIMWI nchini.

Maoni